-
Mshauri wa IRGC: Uwezo mkubwa wa ulinzi wa Iran bado haujaonyeshwa
Jul 07, 2025 03:03Mshauri mwandamizi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, Brigedia Jenerali Ebrahim Jabbari amesema kuwa silaha, zana za kijeshi na vituo vingi vya ulinzi vya Iran bado havijaonyeshwa na kuwekwa paruwanja.
-
Iran: Ugaidi wa kijeshi wa Israel ni pigo kwa diplomasia, NPT
Jul 06, 2025 14:48Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi amelaani uvamizi na hujuma zilizofanywa hivi karibuni na Marekani na Israel dhidi ya Iran, na kuzieleza kuwa pigo kubwa kwa diplomasia, utawala wa sheria na Mkataba wa Kuzuia Uzalishaji na Uenezaji wa Silaha za Nyuklia (NPT).
-
Umuhimu wa vikao na mashauriano aliyofanya Rais wa Iran katika mkutano wa ECO
Jul 06, 2025 09:36Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambaye alikuweko nchini Jamhuri ya Azerbaijan alikohudhuria mkutano wa Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi, ECO, alikutana na viongozi wa nchi zingine wanachama wa jumuiya hiyo, wakabadilishana Mawazo kuhusu matukio ya kikanda na namna ya kupanua ushirikiano kati ya pande mbili.
-
Waislamu leo wanakumbuka A'shura, siku ya kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume, Imam Hussein AS
Jul 06, 2025 04:39Jumapili ya leo ya tarehe 6 Julai inasadifiana na mwezi kumi Muharram 1447 Hijria, siku ya A'shura ya kukumbuka kuuliwa shahidi mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, mmoja wa mabwana wawili wa vijana wa peponi, Imam Hussein AS.
-
Ayatullah Khamenei aongoza majlisi ya maombolezo ya usiku wa A'shura mjini Tehran
Jul 05, 2025 23:48Shughuli ya maombolezo ya usiku wa Ashura ilifanyika jioni ya jana Jumamosi katika Husseiniya ya Imam Khomeini mjini Tehran, ikihudhuriwa na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei na mkusanyiko mkubwa wa watu wa matabaka mbalimbali.
-
Telegraph: Iran ilipiga na kuharibu kambi 5 za kijeshi za Israel
Jul 05, 2025 23:47Gazeti la Telegraph la Uingereza limefichua kwamba makombora ya Iran yalipiga moja kwa moja vituo vitano vya jeshi vya Israel wakati wa vita vya hivi majuzi vya siku 12, lakini Tel Aviv inaendelea kuficha na kuchuja habari za hasara zilizosababishwa na makombora ya Iran.
-
Iran yaghariki katika maomboleza ya Tasua ya Imam Hussein AS
Jul 05, 2025 11:56Mamilioni ya Waislamu nchini Iran wamejiunga na wenzao duniani kote kuadhimisha Tasu'a, siku moja kabla ya maadhimisho ya kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW).
-
Takht-Ravanchi: Iran inaendelea kurutubisha uranium na inaunga mkono diplomasia
Jul 05, 2025 07:55Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran katika Masuala ya Kisiasa amesema kuwa licha ya kutokuwa na imani na Washington kufuatia mashambulizi ya Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran, bado milango ya diplomasia iko wazi. Majid Takht-Ravanchi amesisitiza kuwa: Iran itaendelea kurutubisha madini ya uranium.
-
Iran: Marekani itashindwa kumuokoa Netanyahu na kipigo kijacho cha ‘kupoozesha’
Jul 05, 2025 04:04Mkuu wa Majeshi ya Iran Meja Jenerali Abdolrahim Mousavi ameapa kuwa vikosi vya ulinzi vitatoa jibu la “mapigo ya kupoozesha” kwa uchokozi mwingine wowote mpya wa kijeshi utakaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel; na akaonya kwamba, mapigo hayo yatakuwa makali kiasi cha kuifanya hata Marekani ishindwe kumuokoa Netanyahu, waziri mkuu wa utawala huo bandia aliyeamuru kuanzishwa vita dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Pakistan yasisitiza uungaji mkono wa nchi hiyo kwa Iran
Jul 05, 2025 00:45Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif, amesisitiza uungaji mkono usioyumba wa nchi yake kwa umoja wa ardhi na mamlaka ya kujitawala ya Iran.