-
Marasimu ya Arubaini ya kumuenzi Kiongozi shahidi wa Iran na familia yake yafanyika Musalla wa Imam Khomeini, Tehran
Aug 18, 2026 15:39Sambamba na kutimia siku arubaini tangu kufanyika mazishi ya kihistoria ya kiongozi wa Iran aliyeuliwa shahidi, shughuli ya kumbukumbu ya kumuenzi kiongozi huyo shahidi na familia yake imefanyika leo katika eneo la Swala (Mosalla) la Imam Khomeini (RA) mjini Tehran.
-
Pezeshkian: Ustahimilivu, umoja, na matumaini ni nguzo ya Iran kukabiliana na vitisho vya nje
Aug 18, 2026 11:43Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesema vita vya Iraq dhidi ya Iran, vinavyofahamika nchini Iran kama Vita vya Kujihami Kutakatifu, vina somo muhimu ambalo ni ustahimilivu, umoja, na matumaini.
-
Qalibaf: Iran italipiza kisasi damu ya Kiongozi Shahidi
Aug 18, 2026 11:41Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, ameahidi kwamba Jamhuri ya Kiislamu haitaruhusu damu ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyeuawa shahidi, Ayatollah Sayyid Ali Khamenei, na mashahidi wengine wa uvamizi wa Marekani na Israel dhidi ya taifa hili “kupotea bila kulipiziwa kisasi.”
-
Kamanda: Iran ilitungua ndege zaidi ya 200 za adui katika Uvamizi wa Marekani na Israel
Aug 18, 2026 11:38Naibu Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema kuwa mifumo ya ulinzi wa anga ya Iran ilitungua ndege za adui zaidi ya 200, zikiwemo ndege zisizo na rubani (drones) na ndege zenye marubani, wakati wa uvamizi wa hivi karibuni wa Marekani na Israel.
-
Iran yalaani kauli ya waziri wa Israel, Ben-Gvir ya kuhamasisha mauaji dhidi ya Wapalestina, Gaza
Aug 18, 2026 03:27Mwanadiplomasia mwandamizi wa Iran ameeleza ghadhabu yake baada ya waziri mmoja wa itikadi kali wa utawala wa Kizayuni wa Israel kushauri kwamba utawala huo unapaswa kuwaua Wapalestina wa Ukanda wa Gaza kwa misingi ya “kiwango cha mauaji ya kila usiku.”
-
Baghaei: Iran haibadili sera zake kwa kushinikizwa na kuainishiwa muda
Aug 17, 2026 12:36Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haibadilishi sera zake kutokana na shinikizo au muda wa mwisho uliowekwa.
-
Meja Jenerali Hatami: Ni muhali kwa vituo vya kijeshi vya Marekani kurejea katika hali ya awali
Aug 17, 2026 12:02Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran, Meja Jenerali Amir Hatami amesema Marekani haina tena ruhusa wala haki ya kuingia katika Ghuba ya Uajemi, Bahari ya Oman na Mlango Bahari wa Hormuz, akisisitiza kuwa vituo vya kijeshi vya Marekani katu haviwezi kurejea katika hali iliyokuwepo awali.
-
Malaysia: Iran inapaswa kupongezwa kwa kusimama kidete dhidi ya mashambulizi ya Marekani
Aug 17, 2026 10:37Waziri Mkuu wa Malaysia, Anwar Ibrahim amesema msimamo na azma iliyoonyeshwa na Iran katika kukabiliana na mashambulizi ya kijeshi ya Marekani unastahili pongezi.
-
Kamanda wa IRGC aonya: Adui ajiandae na "mshtukizo wa kimkakati" wa mashambulizi ya Iran
Aug 17, 2026 06:10Kamanda mwandamizi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ameonya kwamba, japokuwa hatua za kijeshi za Iran hadi sasa zimebaki kuwa za kujihami tu tangu ulipoanzishwa uadui wa kijeshi dhidi ya taifa hili, lakini vikosi vya jeshi vimejiandaa kikamilifu kuchukua hatua ya kushambulia endapo italazimu, huku akiwaonya maadui kutarajia "mshtukizo wa kimkakati."
-
Majeshi ya Iran yaapa kutorudi nyuma hadi Marekani na Israel zitaposhindwa kikamilifu
Aug 16, 2026 12:49Kamandi Kuu ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeapa kutorudi nyuma hata kidogo hadi pale haki za kisheria za nchi zitakapopatikana kikamilifu na wavamizi, yaani Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel, watakapokabiliwa na kipigo cha kukomesha katika eneo hili.