-
Araghchi: Mazungumzo ya kiufundi kati ya Iran na Marekani yataanza Jumatano nchini Oman
Apr 20, 2025 02:03Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Abbas Araghchi ameashiria kumalizika kwa duru ya pili ya mazungumzo yasiyo ya ana kwa ana ya nyuklia kati ya Iran na Marekani yaliyofanyika jana Jumamosi mjini Rome, Italia na kueleza kwamba, mazungumzo ya kiufundi katika ngazi ya wataalamu yataanza siku ya Jumatano nchini Oman.
-
Iran: Utawala wa Kizayuni ndio kizuizi pekee kwa Asia Magharibi kuwa eneo lisilo na silaha za nyuklia
Apr 20, 2025 02:01Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Abbas Araghchi amesema utawala wa Kizayuni wa Israel ndio kizuizi pekee kwa Asia Magharibi kuwa eneo lisilo na silaha za nyuklia, akionya kwamba utawala huo unaokalia ardhi kwa mabavu unachochea chuki dhidi ya Iran huku wenyewe ukiendeleza mauaji ya kimbari katika eneo hili.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Israel haina uthubutu wa kutushambulia
Apr 19, 2025 23:25Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "si Israel pekee ambayo haina uthubutu wa kutushambulia, lakini hata Marekani pia haikubali kubahatisha kujiingiza kwenye chokochoko hatari kama hiyo."
-
Press TV: Duru ya pili ya mazungumzo ya Iran na Marekani imefanyika Rome katika 'anga chanya'
Apr 19, 2025 11:02Duru ya pili ya mazungumzo ya nyuklia yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani imefanyika katika mji mkuu wa Italia, Rome leo Jumamosi katika "anga chanya". Hayo yameelezwa na ripota wa chaneli ya televisheni ya Press TV.
-
Mwito wa Iran kwa jamii ya kimataifa wa kuzingatiwa hali ya Gaza
Apr 19, 2025 10:46Esmail Baghaei, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa mwito kwa jamii ya kimataifa kuzingatia kwa uzito jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya watu wa Gaza.
-
Baghaei: Israel imevunja rekodi zote za mauaji ya watoto duniani
Apr 19, 2025 09:43Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, mauaji ya watoto yanayofanywa na Israel huko Ghaza yamevunja rekodi zote duniani na kwamba huo ni uhalifu wa kivita, ni jinai dhidi ya ubinadamu na ni mauaji ya umati kwa mujibu wa sheria za kimataifa.
-
Pezeshkian: Iran yajitahidi kutatua migogoro na kukuza Amani
Apr 18, 2025 23:18Rais Masoud Pezeshkian wa Iran, amesisitiza kuwa serikali yake imejikita katika kutatua migogoro na kukuza amani, huku akieleza kuwa juhudi hizo hazitategemea matokeo ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Marekani.
-
Araqchi: Uhusiano wa Iran na Russia ni imara na wa kimkakati
Apr 18, 2025 22:53Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araqchi ameutaja uhusiano wa Iran na Russia kuwa ni imara mno na kwamba Moscow ni mshirika mkuu na wa kistratijia wa Iran.
-
Ayatullah Khatami: Iran haishurutishwi wala haisalimu amri
Apr 18, 2025 11:03Khatibu wa Swala ya leo ya Ijumaa katika jiji la Tehran ameashiria mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani kuhusu suala la nyuklia na kuondolewa vikwazo na akasema: "Katika mazungumzo hayo, tunapasa kuwa makini na tusimtegemee yoyote isipokuwa Mwenyezi Mungu, tusichoke kupambana, na tusifungamanisha hatima yetu na mazungumzo."
-
Pezeshkian: Jeshi ni ngome imara ya serikali na taifa la Iran
Apr 18, 2025 11:02Rais wa Iran amelitaja jeshi la Iran kuwa ni ngome imara ya serikali na taifa, chanzo cha heshima ya taifa, ni msaada kwa taifa na serikali.