-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu alihimiza taifa la Iran kusimama kidete katika vita vya kisaikolojia vya adui
Aug 15, 2024 06:35Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Ali Khamenei, amezungumzia hila na njama za wasiolitakia mema taifa la Iran katika kuanzisha vita vya kisaikolojia na kutaka kulirudisha nyuma katika nyuga mbalimbali na kusema, utambuzi wa uwezo wa ndani na kuepuka kutia chumvi nguvu za maadui ndiyo njia pekee ya kukabiliana na njama hizo.
-
Jenerali Ghorbani: Vikwazo vimeimarisha mfumo wa kijeshi wa Iran
Aug 15, 2024 04:15Naibu Mratibu wa Kikosi cha Nchi Kavu cha Jeshi la Iran amesema kuwa vikwazo vya kikatili dhidi ya Iran havijakuwa na matokeo mengine ghairi ya kuimarisha mifumo ya kijeshi ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Baadhi ya Wairani kwenda Arubaini, Iraq kwa njia ya bahari
Aug 15, 2024 04:13Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefungua njia ya baharini kutoka Bandari ya Khorramshahr, Magharibi mwa Iran hadi Bandari ya Basra nchini Iraq kwa ajili ya safari ya majini ya Mazuwari wa Kiirani wanaoenda kushiriki Arubaini ya Imam Hussein AS.
-
Iran yatuma barua za malalamiko kwa maafisa wa haki za binadamu wa UN
Aug 14, 2024 11:27Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa mjini Geneva Uswisi amewatumia barua kwa nyakati tofauti maafisa wa haki za binadamu akibainisha malalamiko makubwa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa hatua na sera zisizo z akibinadamu za utawala wa Kizayuni na hasa mauaji ya kigaidi ya Ismail Haniyeh kiongozi wa kisiasa wa Hamas.
-
Iran imetoa mikopo ya dola bilioni 28.7 kwa biashara, viwanda na familia katika kipindi cha miezi minne
Aug 14, 2024 11:26Takwimu za Benki Kuu ya Iran zinaonyesha kuwa kaya nchini zilipata asilimia 22.7 ya jumla ya mikopo iliyotolewa na mfumo wa benki nchini katika kipindi cha miezi minne hadi Julai 21.
-
Kiongozi Muadhamu atilia mkazo wajibu wa kusimama imara mbele ya vita vya kisaikolojia vya adui
Aug 14, 2024 09:00Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametilia mkazo wajibu wa kusimama imara kukabiliana na vita vya kisaikolojia vya adui akisema kuwa, wanaoendesha vita hivyo dhidi ya Iran wanajaribu kuzusha hofu na kulifanya taifa hili lilegeze kamba na lirudi nyuma katika nyuga tofauti.
-
Bagheri Kani: Uvamizi wa Wazayuni katika Msikiti wa Al-Aqsa unalenga kuzidisha mivutano
Aug 14, 2024 04:07Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema uvamizi wa baadhi ya mawaziri wa serikali ya utawala bandia wa Israel na walowezi wa Kizayuni katika msikiti wa al Aqsa ni hatua ya kichochezi inayolenga kushadidisha mivutano na ukosefu wa amani katika eneo.
-
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran kwa mnasaba wa maadhimisho ya " Siku ya Muqawama wa Kiislamu"
Aug 14, 2024 03:52Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetoa taarifa na kupongeza kuadhimishwa "Siku ya Muqawama wa Kiislamu."
-
Iran: Hatuhitaji kibali kwa ajili ya kulinda usalama wa taifa na kumzuia adui
Aug 14, 2024 00:57Iran imesisitiza "haki yake inayotambuliwa" ya kutetea mamlaka ya kitaifa na kujenga kizuizi dhidi ya Israel kama chanzo cha ugaidi katika eneo hili, ikisema kuwa taifa hili halihitaji ruhusa kutoka kwa mtu yeyote" kuhusu suala hilo.
-
Kukanushwa tuhuma za Marekani dhidi ya Iran
Aug 13, 2024 22:52Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema, Marekani ndiyo muungaji mkono na muenezaji mkuu wa ugaidi katika eneo na dunia.