-
Iran yaiambia Jordan: Mnataraji tusubiri hadi lini kutomjibu mchokozi?!
Sep 04, 2026 10:52Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amejibu matamshi ya hivi karibuni ya waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Jorda kwa kumuuliza: Mnataraji Jamhuri ya Kiislamu ya Iran isubiri hadi lini kutomjibu mchokozi ambaye haheshimu haki ya kujitawala nchi za Kiarabu wala haki za Iran?
-
Reuters: Marekani ndiyo iliyoshambulia sherehe ya harusi nchini Iran
Sep 04, 2026 10:44Baada ya kukiri New York Times, sasa ni zamu ya shirika la habari la Reuters kukiri na kuripoti kwamba, lina ushahidi wa wataalamu wanne wa silaha wanaothibitisha kuwa Marekani ndiyo iliyoshambulia moja kwa moja wananchi waliokuwa kwenye sherehe ya harusi huko Sirik kusini mwa Iran.
-
Qatar imethibitisha kuwa mashambulio ya Iran ndani ya ardhi ya nchi hiyo yalilenga vituo vya kijeshi tu vya Marekani
Sep 04, 2026 03:22Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei, ameashiria hati rasmi ya Qatar iliyowasilishwa kwa Umoja wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU) ikithibitisha kwamba operesheni halali za kujihami za Jamhuri ya Kiislamu dhidi ya vikosi vya Marekani vilivyoko katika ardhi ya Qatar zilielekezwa kwenye vituo vya kijeshi tu vya Marekani.
-
Meja Jenerali Vahidi: Damu isiyo na hatia ya mashahidi madhulumu wa Kohestak haitapotea
Sep 04, 2026 03:20Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ametuma ujumbe maalumu na kusema kuwa: Damu isiyo na hatia ya mashahidi waliouliwa kidhulma na magaidi wa Kimarekani huko Kohestak haitapotea kamwe na wahusika wakiwemo makamanda waliofanya jinai hiyo ya kivita wataburuzwa mahakamani.
-
Baada ya shambulio harusini; IRGC yasema: Viongozi wa US wanapasa kuwajibishwa kwa jinai za kivita
Sep 03, 2026 10:17Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) limetangaza kuwa Washington lazima iwajibishwe kwa jinai za kivita zilizofanywa na wanajeshi magaidi wa Marekani katika Mkoa wa Hormozgan kufuatia shambulio la anga lililolenga sherehe ya harusi.
-
Kuanzia shule ya Minab hadi harusi ya Kuhestak: Raia waendelea kuwa wahanga wa ukatili wa Marekani
Sep 03, 2026 06:40Jioni ya Jumanne, jeshi la Marekani lilishambulia kinyama sherehe ya harusi katika bandari ya Kuhestak, katika Wilaya ya Sirik kusini mwa Iran. Makumi ya watu waliuawa shahidi na kujeruhiwa; huku wanawake na watoto wakiwa miongoni mwa wahanga.
-
Qalibaf: Iran na kambi ya Muqawama wako katika njia moja dhidi ya ubeberu
Sep 03, 2026 03:26Spika wa Bunge la Iran amesema kuwa Iran na kambi ya Muqawama wako katika njia moja kukabiliana na ubeberu.
-
Iran: Baraza la Usalama la UN lilaani shambulio la Marekani lililoua raia kwenye sherehe ya harusi
Sep 03, 2026 03:19Iran imeliitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulaani shambulio la Marekani lililolenga nyumba ya makazi iliyokuwa ikiandaa sherehe ya harusi kusini mwa Jamhuri ya Kiislamu, ambalo limesababisha kuuawa shahidi wa raia watano, akiwemo mtoto wa miaka minne, na kuwajeruhi zaidi ya watu 70 wengine.
-
IRGC yapiga makao ya kamandi ya Marekani na eneo la kuegeshea droni huko Kuwait
Sep 02, 2026 12:57Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) limesema kuwa vikosi vyake vimeshambulia makao makuu ya kamandi na makazi ya wanajeshi wa Marekani katika Kituo cha Jeshi la Anga cha Ali Al-Salem nchini Kuwait, na kuteketeza ghala la ndege zisizo na rubani (droni) na eneo la maandalizi ya kurushia ndege hizo. Shambulizi hilo limeharibu idadi kadhaa ya ndege zisizo na rubani za jeshi la kigaidi la Marekani.
-
Qalibaf: Marekani ‘inaua kama Shetani’: Alaani shambulio dhidi ya sherehe ya harusi kusini mwa Iran
Sep 02, 2026 12:55Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf amelaani shambulio la Marekani dhidi ya sherehe ya harusi kusini mwa Iran, akisema kuwa kulenga raia katika shule, ukumbi wa michezo na sherehe ya harusi kunaonyesha namana Washington inavyotenda na kuua "kama Shetani."