-
Hizbullah ya Lebanon: Muqawama utalipiza kisasi cha mashahidi wake
Nov 25, 2025 07:33Mwanachama mmoja wa ngazi za juu katika Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa harakati hiyo ya muqawama italipiza kisasi cha mashahidi wake na kwamba irada yake kamwe haitadhoofishwa.
-
Mahmood Mamdani: Israel ni dola la wavamizi, inafanya majaribio ya silaha zake juu ya vichwa vya watu wa Gaza
Nov 25, 2025 07:33Msomi na mwanafikra mashuhuri raia wa Uganda, Mahmood Mamdani, ambaye ni baba wa Muislamu wa kwanza kushinda nafasi ya umeya wa New York huko Marekani, Zohran Kwame Mamdani, ameishutumu Israel kuwa ni "nguvu ya uchokozi ambayo imepoteza hisia zote za maadili," na kwamba hakuna anayeamini kwamba kile inachofanya huko Gaza ni "kujilinda" kama inavyodai.
-
Larijani: Ushirikiano wa Iran na Pakistan unachangia amani ya kikanda
Nov 25, 2025 07:30Ali Larijani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran (SNSC), amesema ushirikiano kati ya Tehran na Islamabad katika nyanja mbalimbali unaimarisha amani na utulivu wa kieneo, na kuangazia nafasi muhimu ya Pakistan katika uwanja huo.
-
Kwa nini mkataba wa gesi kati ya Israel na Misri unakaribia kusambaratika?
Nov 25, 2025 06:52Hitilafu za kisiasa na kiusalama kati ya utawala ghasibu wa Israel na Misri zimechukua zimefikia katika uga wa kiuchumi, na sasa zimefikisha mkataba mkubwa zaidi wa gesi kati ya Tel Aviv na Cairo kwenye ukingo wa kusambaratika.
-
Afisa wa Umoja wa Mataifa: Hali bado ni mbaya huko Gaza
Nov 25, 2025 04:00Ramiz Alakbarov, Naibu Mratibu Maalumu wa Umoja wa Mataifa wa Mchakato wa Amani wa Mashariki ya Kati, ameonya kwamba hali katika Ukanda wa Gaza "inaendelea kuwa mbaya," na kusema kuwa familia nyingi haziwezi kumudu kununua kuku na nyama licha ya upatikanaji wa bidhaa za msingi za chakula na kuboreshwa kwa bei za bidhaa hizo.
-
Wakuu wa usalama Nigeria waripoti maendeleo katika operesheni ya kuokoa wanafunzi waliotekwa nyara
Nov 25, 2025 03:59Maafisa wa jeshi la Nigeria wametangaza kuwa kumepigwa hatua nzuri za maenedelea katika jitihada za kukomboa mamia ya wanafunzi wa kike na walimu wao kadhaa waliotekwa nyara na kundi la watu waliokuwa na silaha katika jimbo la Niger, kaskazini mwa nchi hiyo.
-
Hemedti atangaza kusitisha mapigano kwa upande mmoja, raia wanaendelea kukimbia makazi yao Sudan
Nov 25, 2025 03:09Kamanda wa waasi wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), Mohamed Hamdan Dagalo “Hemedti”, ametangaza kusitisha mapigano ya ndani kwa kipindi cha miezi mitatu kwa "sababu za kibinadamu", ambako kunajumuisha kusitishwa uhasama; siku moja baada ya mkuu wa Baraza la Mpito la Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, kukaataa pendekezo la Marekani kwa ajili ya kusitisha mapigano.
-
Umoja wa Mataifa: Mwanamke mmoja huuliwa kila baada ya dakika 10
Nov 25, 2025 03:08Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa jana Jumatatu ilisema kwamba karibu wanawake 50,000 waliuawa na jamaa zao mwaka wa 2024, kwa kiwango cha mwanamke mmoja kila baada ya dakika 10, na kuelezea masikitiko yake kwamba hakuna maendeleo yoyote yaliyopatikana katika kupambana na mauaji ya wanawake.
-
IEBC yawataka wanasiasa wa Kenya wasichochee machafuko na uvunjivu wa amani
Nov 25, 2025 03:04Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya (IEBC), imewataka wanasiasa kuelekeza nguvu zao katika kuhimiza amani na utulivu, badala ya kutoa matamshi yanayoweza kuchochea taharuki miongoni mwa wananchi.
-
IRGC: Mauaji ya kamanda wa Hizbullah yamefichua udhaifu wa Israel mbele ya Muqawama
Nov 24, 2025 23:42Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) limesema kuwa mauaji ya kikatili yaliyofanywa na Israel dhidi ya kamanda wa ngazi za juu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon yamefichua “udhaifu” wa utawala huo mbele ya Mhimili wa Muqawama.