-
Kura ya maoni: Wamarekani wengi wanapinga hatua za kijeshi dhidi ya Venezuela
Nov 24, 2025 23:14Kura ya maoni iliyofanywa na CBS News ikishirikiana na kampuni ya utafiti ya YouGov imeonyesha kuwa Wamarekani wengi wanapinga hatua zozote za kijeshi dhidi ya Venezuela.
-
Familia za watoto waliotekwa nyara Nigeria zachanganyikiwa kutokana na kukaririwa vitendo hivyo mashuleni
Nov 24, 2025 23:13Familia za wanafunzi waliotekwa nyara nchini Nigeria zimenasa kati ya matumaini na kukatishwa tamaa kutokana na vitendo vya kukaririwa vya utekaji nyara wanafunzi wakiwa mashuleni.
-
Hamas: Ukiukaji wa Israel wa makubaliano ya kusitisha mapigano ya Gaza unadhoofisha makubaliano hayo
Nov 24, 2025 23:12Hazem Qassem, msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) huko Gaza, amesema kwamba ujumbe wa harakati hiyo umefanya mazungumzo na maafisa wa Misri huko Cairo kujadili awamu inayofuata ya makubaliano ya kusitisha mapigano.
-
Rais wa Korea Kusini: Mifumo ya kimataifa ya AI inapasa kuhakikisha mataifa yote yanapa teknolojia hiyo kwa usawa
Nov 24, 2025 23:10Rais wa Korea Kusini, Lee Jae Myung amesema kuwa mifumo ya kimataifa ya akili mnemba (AI) inapasa kuhakikisha kuwa mataiafa yote yanapata teknolojia hiyo kwa usawa.
-
Mamluki wa kigeni wana jukumu gani katika kuchochea vita nchini Sudan?
Nov 24, 2025 23:09Kamati ya Uchunguzi wa Haki za Binadamu imetangaza kuhusu ushirikiano uliopo kati ya mamluki wa kigeni na Vikosi vya Msaada wa Haraka vya Sudan RSF katika vita vya ndani nchini humo.
-
Al Burhan akataa pendekezo la Marekani, alitaja kuwa baya zaidi kwa ajili ya utatuzi wa mgogoro wa Sudan
Nov 24, 2025 11:54Mkuu wa Baraza la Utawala wa Mpito nchini Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, amekataa pendekezo lililowasilishwa na mshauri wa Rais wa Marekani kuhusu masuala ya Kiarabu na Afrika, Massad Boulos, juu ya utatuzi wa mgogoro wa Sudan.
-
Mohsein Rezaei: Israel inaharakisha anguko lake kwa kuwauwa makamanda wa Muqawama
Nov 24, 2025 11:53Kamanda Mkuu wa zamani wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ameonya kuwa mauaji yanayofanywa na utawala wa Israel dhidi ya makamanda wa Muqawama yanaharakisha kuangamia utawala huo.
-
Tanzania kuanza kujenga bandari yenye thamani ya dola bilioni 10 mwezi Desemba
Nov 24, 2025 11:44Tanzania itaanza ujenzi wa bandari mpya mashariki mwa nchi mwezi Desemba mwaka huu na hivyo kumaliza muongo mmoja wa ucheleweshaji kutokana na pingamizi la serikali kwa masharti ya awali ya kandarasi.
-
UNRWA yatahadharisha kuhusu njaa ya kupanga huko Gaza
Nov 24, 2025 11:32Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limetahadharisha kuhusu hali mbaya ya njaa, kusitishwa huduma muhimu na tishio la maisha ya mamilioni ya wakimbizi wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza, likitaja ukosefu mkubwa wa rasilimali za kifedha na vikwazo vikubwa vya utawala wa Israel.
-
Raia wengi wakimbia makazi yao baada ya magaidi kuteka nyara mabinti 13 katika jamii ya Borno, Nigeria
Nov 24, 2025 11:09Wimbi la hofu limeikumba jamii ya Borno, na raia wengi wameanza kuondoka majumbani mwao leo Jumatatu, siku mbili baada ya ISWAP, tawi la kundi Boko Haram, kuwateka nyara mabinti 13 wenye umri wa miaka 15 hadi 20.