-
Uchaguzi Mkuu unakaribia Uganda, Polisi wazuia wapinzani kufanya kampeni Arua
Nov 20, 2025 06:46Huku Uchaguzi Mkuu ukizidi kukaribia nchini Uganda, Jeshi la Polisi la nchi hiyo limekizuia chama cha upinzani cha Jukwaa la Umoja wa Kitaifa NUP kuingia katika eneo la kampeni za uchaguzi lililokuwa limepangwa kabla kwenye mji muhimu wa Arua wa kaskazini mwa Uganda jana Jumatano.
-
UNRWA yaonya kuhusu mgogoro wa kibinadamu wa Ghaza majira ya baridi kali
Nov 20, 2025 06:45Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la UNRWA amesema kwamba, usitishaji mapigano haujawa na athari yoyote katika kuboresha hali ya watu wa Ghaza, na kwamba mateso makubwa ya binadamu katika ukanda huo yanaendelea na misaada inayoingizwa ni midogo sana hasa wakati huu wa kuwadia msimu wa baridi kali.
-
Wanawake wajawazito Sudan wafanya safari ngumu za kukimbia machafuko ya El-Fasher
Nov 20, 2025 06:44Nadra Mohamed Ahmed alikuwa na ujauzito wa miezi saba wakati alipokimbia machafuko na mauaji katika mji wake wa El-Fasher nchini Sudan. Baada ya kutembea kwa karibu kilomita 40 katika barabara zisizo salama na watoto wake wawili, alipata usafiri salama hadi kwenye makazi yake mapya.
-
Araghchi: Hatutakubali kwa namna yoyote ile kushusha urutubishaji urani hadi kiwango cha sifuri
Nov 20, 2025 03:23Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Sayyid Abbas Araghchi amesema: "hatutakubali kwa namna yoyote ile kushusha urutubishaji wa urani hadi kiwango cha sifuri kwa sababu hili limekuwa ni jambo la fakhari na heshima kwa taifa, tumetumia gharama nyingi sana za kimaada na kimaanawi kwa ajili yake, na tumepoteza wanasayansi kadhaa waliouawa shahidi kwa ajili ya kulidumisha".
-
Israel yafanya mashambulio ya kinyama Ghaza, yaua Wapalestina 28 na kujeruhi 77
Nov 20, 2025 02:39Wapalestina wasiopunguua 28 wameuawa shahidi katika wimbi jipya la mashambulizi ya kinyama yanayofanywa na jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel kwenye Ukanda wa Ghaza, yakiwa ni moja ya ukiukaji mkubwa zaidi wa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyosimamiwa na Marekani na kuanza kutekelezwa mwezi uliopita wa Oktoba.
-
Watu 70 hawajulikani waliko baada ya boti kuzama mkoani Kasai, DRC
Nov 20, 2025 02:39Watu wapatao 70 hawajulikani walipo baada ya boti kuzama mtoni katika Mkoa wa Kasai katikati mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
WHO: Ukatili dhidi ya wanawake ungali ni janga kubwa la haki za binadamu
Nov 20, 2025 02:38Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) pamoja na wadau wa Umoja wa Mataifa wametoa ripoti muhimu inayoonyesha kuwa ukatili dhidi ya wanawake ungali ni janga kubwa la haki za binadamu, kwa sababu takwimu za zaidi ya miaka 20 zinaonesha kutokuwepo kwa hatua kubwa zilizopigwa katika kupunguza ukatili huo.
-
Trump na Meya mteule wa New York, Mamdani kukutana White House Ijumaa
Nov 20, 2025 02:38Rais wa Marekani Donald Trump amesema, atakutana na Meya mteule wa Jiji la New York Zohran Mamdani katika Ikulu ya White House siku ya Ijumaa.
-
Mgogoro wa Sahel: Tishio la Kikanda au Hatari ya Kimataifa?
Nov 20, 2025 02:11Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ametahadharisha kuhusu ukuaji na upanukaji wa makundi ya kigaidi barani Afrika na kutangaza kuwa: "Hali ya usalama, hasa katika Afrika Magharibi na eneo la Sahel, inazidi kuwa mbaya siku hadi siku."
-
Afrika Kusini imejiandaa kuwa mwenyeji wa mkutano wa G20 uliosusiwa na Marekani
Nov 19, 2025 23:49Afrika Kusini inajiadaa kuwa mwenyeji wa mkutano wa G20, unaowakutanisha viongozi kutoka mataifa tajiri duniani, kujadili masuala mbalimbali yakiwemo ya kiuchumu na kisiasa. Maandalizi ya mkutano huo utakaofanyika sikuu za Jumamosi na Jumapili ijayo yamekamilika.