-
Araqchi na Lavrov wafanya mashauriano ya simu kuhusu Gaza
Nov 12, 2025 23:09Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Russia wamefanya mazungumzo kwa njia ya simu na kubadilishana mawazo kuhusiana na masuala mbalimbali yakiwemo ya uhusiano wa pande mbili.
-
Ujerumani ni muuzaji mkubwa wa pili wa silaha kwa Israel
Nov 12, 2025 23:07Imeelezwa kuwa, Ujerumani inashika nafasi ya pili duniani kwa kuuuzia silaha utawala haramu wa Israel unaofanya mauaji ya kinyama dhidi ya Wapalestina.
-
UNICEF: Watu wanane kati ya kumi nchini Afghanistan wanakunywa maji machafu
Nov 12, 2025 23:07Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limetangaza kuwa, zaidi ya nusu ya vyanzo vya maji vya Afghanistan vimekauka.
-
Umoja wa Mataifa wataka uchunguzi kwa mauaji Tanzania
Nov 12, 2025 23:06Umoja wa Mataifa umetowa wito wa kufanyika uchunguzi kwa kile kinachodaiwa kuwa vifo vya mamia ya watu katika machafuko ya kupinga uchaguzi nchini Tanzania.
-
Kujiunga Wazungu na harakati ya kuisusia Israel; mabadiliko ya kweli au mashinikizo ya umma?
Nov 12, 2025 23:05Harakati ya kususia bidhaa za Israeli (BDS) inazidi kupata nguvu kote duniani, tena kwa kasi kubwa, na watu binafsi na taasisi mbalimbali kote ulimwenguni zinajiunga nayo kwa lengo la kuongeza mashinikizo kwa Israel. Katika uamuzi muhimu zaidi wa hivi karibuni, ni nchi ya Ulaya ya Uholanzi kutangaza kwamba inaandaa sheria ya kupiga marufuku kuingiza nchini humo bidhaa zinazozalishwa katika vitongoji haramu vya walowezi wa Kizayuni huko Palestina.
-
FAO na WFP zatoa indhari: Baa la njaa linazidi kuongezeka katika sehemu 16 duniani
Nov 12, 2025 09:33Ripoti mpya ya pamoja ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) la na Mpango wa Chakula Duniani (WFP) iliyotolewa leo Jumatano zimetahadharisha kuwa, hali ya ukosefu wa usalama wa chakula inazidi kuwa mbaya katika maeneo 16 yenye janga la njaa duniani, huku mamilioni ya watu wakiwa katika hatari ya kupatwa na janga hilo katika kipindi cha kati ya Novemba 2025 na Mei 2026.
-
HAMAS: Silaha za Muqawama haziwezi kujadiliwa kabla ya kuundwa kwanza nchi ya Palestina
Nov 12, 2025 08:40Osama Hamdan, kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS, amesisitiza kwamba, silaha za Muqawama ni suala lisiloweza kujadiliwa kabla ya kuundwa nchi dola ya Palestina na akabainisha kuwa, lengo la kisiasa la Muqawama litabaki kuwa ni kuikomboa ardhi, kuundwa nchi huru ya Palestina ambayo mji mkuu wake ni Baitul-Muqaddas na kuwepo hakikisho la kurejea wakimbizi.
-
Museveni aonya: Vita vitatokea Afrika ikiwa nchi zisizo na bandari zitashindwa kufikia Bahari ya Hindi
Nov 12, 2025 08:08Katika kauli iliyotafsiriwa kama onyo lililolenga nchi jirani, Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameonya kuhusu uwezekano wa kutokea vita katika siku zijazo endapo nchi za Afrika ambazo hazina bandari zitaendelea kunyimwa haki ya kufikia Bahari ya Hindi.
-
Katibu Mkuu wa UN apongeza uchaguzi wa bunge Iraq, ahimiza kuundwa serikali kwa njia ya amani
Nov 12, 2025 07:42Wakati zoezi la kuhesabu kura za uchaguzi wa Bunge la Iraq lingali linaendelea, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewapongeza wananchi wa nchi hiyo kwa ushiriki wao katika uchaguzi huo na kuipongeza pia Tume Huru ya Uchaguzi (IHEC) kwa kuendelesha zoezi hilo kwa ufanisi.
-
UNDP: Familia 9 kati ya 10 Afghanistan zinasamehe matibabu ili kupata mlo huku zikibeba madeni
Nov 12, 2025 07:41Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) limetangaza kuwa, familia tisa kati ya 10 nchini Afghanistan zinakabiliwa na njaa au zinalazimika kubeba madeni huku raia wakimbizi waliorejea hivi karibuni wakijikimu kimaisha kwa tabu katika maeneo yenye hali mbaya ya umaskini mashariki na kaskazini mwa nchi hiyo.