-
Trump amwambia Netanyahu katika malumbano makali ya simu: "Wayahudi wote wamekuchoka"
Jun 26, 2026 11:16Televisheni ya CNN ya Marekani imefichua malumbano makali ya simu baina ya Rais wa Marekani na Waziri Mkuu wa Israel ambapo Donald Trump amemkemea Benjamin Netanyahu, akimwambia: "Wayahudi wote wamekuchoka," huku Marekani ikizidisha mashinikizo kwa ajili ya kufikia makubaliano kuhusu Ukanda wa Gaza.
-
Afrika Kusini yaapa kukabiliana vikali na ukatili dhidi ya wahamiaji
Jun 26, 2026 11:10Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ameapa kukabiliana na jaribio lolote la kuyumbisha taifa wakati wa maandamano yaliyopangwa kufanywa wiki ijayo dhidi ya wahamiaji, huku wimbi la chuki dhidi ya wageni lizidi kuongezeka nchini humo.
-
Timu za uokoaji zinakimbizana na wakati kutafuta manusura chini ya vifusi; huenda 10,000 wameuawa zilzala ya Venezuela
Jun 26, 2026 10:38Baada ya mitetemeko miwili mikubwa ya ardhi kukumba miji kadhaa nchini Venezuela Jumatano jioni, Wavenezuela wamekuwa wakiishi katika hali ngumu, ikiwa ni pamoja na kuhama makazi na kutafuta jamaa zao waliokwama chini ya vifusi, huku makadirio yakisema kwamba idadi ya vifo vilivyosababishwa na mitetemeko hiyo inaweza kuzidi watu 10,000.
-
Iran: Waliohusika na mauaji ya wanafunzi wa shule ya Minab wachukuliwe hatua
Jun 26, 2026 04:21Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amelaani "uhalifu mbaya" uliofanywa na Marekani katika shule ya Msingi ya Shajareh Tayyebeh ya Minab nchini Iran wakati wa mashambulizi ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Jamhuri ya Kislamu, na kutoa wito kwa wahusika wote, wapangaji na viongozi kuwajibishwa kikamilifu, akisisitiza kwamba: "Kumbukumbu ya watoto wa Minab inahitaji haki, uwajibikaji na utekelezaji, si kukaa kimya."
-
Joto kali lasababisha vifo vya zaidi ya watu 212 barani Ulaya
Jun 26, 2026 04:08Nchi kadhaa za Ulaya zimerekodi vifo vya makumi ya watu kutokana na wimbi kubwa la joto, huku kwa uchache watu 212 wakifariki dunia nchini Uhispania, na wengine kadhaa, wakiwemo watoto 3, wakiaga dunia nchini Ufaransa wiki hii.
-
Wafungwa 11 wa kisiasa Tunisia wataka kuanzishwa kambi moja ya upinzani ili kurejesha uhuru
Jun 26, 2026 03:53Wafungwa kumi na mmoja wa Tunisia wameyataka makundi ya upinzani nchini humo "kuungana ili kurejesha uhuru na demokrasia" nchini humo.
-
Wamarekani: Waasisi wangekatishwa tamaa na hali ya sasa ya nchi
Jun 26, 2026 03:50Wamarekani wengi wamekatishwa tamaa na serikali yao, wakisema kwamba Waasisi wangesikitishwa sana na hali ya sasa ya kijamii na kisiasa ya Marekani.
-
Polisi yatumia mabomu ya machozi kudhibiti maandamano Kenya
Jun 26, 2026 02:39Polisi nchini Kenya jana walitumia mabomu ya kutoa machozi dhidi ya waandamanaji katika maeneo mbalimbali mjini Nairobi huku makundi yanayoongozwa na vijana yakifanya kumbukumbu ya miaka miwili tangu maandamano ya Gen Z.
-
Ashura; Shule ya Ufahamu na Uaminifu Iliyovuka Mipaka ya Historia
Jun 25, 2026 12:55Ashura; Shule ambayo iliunganika na damu tukufu na kupelekea watu waaminifu 72 kuuawa shahidi, na hivyo kuwa taa ya wongofu wa historia huku wakiwa wamechagua utukufu wa milele kwa ufahamu na mwamko kamili.
-
Rais Pezeshkian: Imam Hussein (a.s.) ametufundisha kusimama dhidi ya dhulma
Jun 25, 2026 10:07Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amesema kuwa, Imam Hussein (a.s.) ametufundisha kusimama dhidi ya dhulma, vishawishi vya madaraka, na tamaa ya maslahi binafsi.