Feb 10, 2024 10:40 UTC
  • Msemaji wa Maulamaa wa Palestina: Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yamebadilisha historia ya dunia

Mkuu wa Baraza la Ushauri na Msemaji wa Baraza Kuu la Maulamaa wa Palestina amesema kuwa, Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran si kwa ajili ya nchi hiyo tu bali ni kwa ajili ya ulimwengu mzima kwani yamebadilisha sura ya historia ya dunia.

Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalipata ushindi tarehe 22 Bahman 1357 Hijria Shamsia iliyosadifiana na tarehe 11 Februari 1979 Milaadia. Mapinduzi hayo yalipata ushindi kutokana na mapambano ya pande zote ya Imam Khomeini MA kwa kushirikiana na matabaka mbalimbali ya wananchi.

Kwa mnasaba wa maadhimisho hayo ambayo mwaka huu yanafikia kileleni kesho Jumapili, Februari 11, 2024, Sheikh Muhammad Saleh al Mauid, amesema leo Jumamosi katika mahojiano na shirika la habari la IRNA kwamba, Mapinduzi ya Kiislamu kwa uongozi wa Imam Khomeini MA yamelifikisha taifa la Iran kwenye hadhi yake linayostahiki kuwa nayo na kwamba mwanachuoni huyo shujaa amefanikiwa kuleta ukombozi huo mkubwa kutokana na muono wake mpana na wa mbali sana.

Imam Khomeini na kadhia ya Quds 

 

Amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran chini ya uongozi wa mwasisi wake yaani Imam Khomeini MA na baadaye chini ya uongozi wa busara na wa kishujaa wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, yamelifikisha taifa la Iran kwenye hadhi na itibari ya hali ya juu kiasi kwamba athari zake zinahisika hivi sasa katika sehemu kubwa ya ulimwengu. 

Msemaji huyo wa Baraza la Maualamaa wa Palestina ameongeza kuwa, jina la Iran leo hii linagonga vichwa vya habari kote duniani na kwa lugha zote ulimwenguni kutokana na msimamo imara wa Jamhuri ya Kiislamu, uhuru na nafasi yake kubwa katika matukio ya dunia.

Tags