Apr 15, 2024 13:47 UTC
  • Mufti Mkuu wa wa Oman
    Mufti Mkuu wa wa Oman

Mufti Mkuu wa wa Oman amekaribisha na kupongeza mashambulizi ya Iran dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Sheikh Ahmad bin Hamad al-Khalili ameandika ujumbe katika ukurasa wake binafsi katika mtandao wa kijamii wa X na kusema: Kilichochapishwa katika vyombo vya habari kuhusu ujasiri wa hatua ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kujibu mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika ubalozi mdogo wa Iran ni jambo la kufurahisha sana, na tunatumai litazaa matunda hivi karibuni.

Mufti wa Oman ameongeza kuwa: Tunapongeza kitendo hiki na vingine mfano wake na tunatumai kuwa vitalinda uwezo na uwepo wa Umma. Kwa sababu nguvu ya kujilinda ni muhimu sana kwa ajili ya kikabiliana na shari, vinginevyo, itaenea na kupanuka.

Sheikh Ahmad al Khalili amesema: Tunatumai kuwa yaliyotokea yatakuwa na uchungu na maumivu kwa Wazayuni na wale waliowasaidia, na tunasubiri kwa hamu kubwa jambo litakalovunja nguvu za Wazayuni, kuzima njama zao na kuwalinda Waislamu na shari yao.