Apr 19, 2024 07:29 UTC
  • Utawala wa Kizayuni una hofu ya kutolewa waranti wa kumkamata Netanyahu

Baraza la Mawaziri la utawala wa Kizayuni limefanya kikao cha dharura kuchunguza uwezekano wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC kutoa waranti wa kukamatwa Benjamin Netanyahu na maafisa wengine wa utawala huo dhalimu wa Israel kwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya Wapalestina huko Ghaza.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB, Channel 12 ya Televisheni ya utawala wa Kizayuni imeripoti kuwa, kuna wasiwasi ndani ya Israel wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai yenye makao yake The Hague kutoa waranti wa kimataifa wa kukamatwa maafisa wakuu wa Israel akiwemo waziri wake mkuu Benjamin Netanyahu.

Netanyahu ameitisha kikao cha dharura kuchunguza uwezekano wa Mahakama ya Kimataifa ya ICC kutoa hati ya kumkamata yeye na maafisa wengine wa Israel kutokana na vita vya Ghaza.

Huku akidai kwamba Israel inakabiliwa na tishio la uwepo wake, Netanyahu ametoa wito wa kuwepo umoja wa makundi yote ya ndani ya Wazayuni kwa ajili ya kukabiliana na hatari hizo.

Kufuatia mashtaka yaliyowasilishwa na Afrika Kusini dhidi ya utawala wa Kizayuni katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki, mahakama hiyo iliutaka utawala wa Kizayuni katika hukumu iliyotoa uchukue hatua za kuzuia mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Ghaza.../

 

Tags