Jumamosi, 05 Disemba, 2020
https://parstoday.ir/sw/news/uncategorised-i65008-jumamosi_05_disemba_2020
Leo ni Jumamosi tarehe 19 Mfunguo Saba Rabiu Thani 1442 Hijria mwafaka na tarehe 5 Desemba 2020 Miladia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 05, 2020 00:47 UTC
  • Jumamosi, 05 Disemba, 2020

Leo ni Jumamosi tarehe 19 Mfunguo Saba Rabiu Thani 1442 Hijria mwafaka na tarehe 5 Desemba 2020 Miladia.

Siku kama ya leo miaka 150 iliyopita, aliaga dunia Alexandre Dumas mwandishi mtajika wa Kifaransa. Mwandishi huyo ambaye ni mashuhuri pia kwa jina la Dumas Baba baada ya kumaliza masomo yake aliajiriwa katika ofisi moja ya kiwanda kama katibu kutokana na kuwa na hati nzuri.***

Alexandre Dumas

 

Katikka siku kama ya leo miaka 146 iliyopita, Iran ilijiunga na Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu. Jitihada za awali za Iran kutaka kujiunga na shirika hilo zinarejea nyuma katika kipindi cha utawala wa Mfalme Nassereddin Shah Qajar. Katika kipindi cha utawala wake, Disemba 1874 Iran iliukubali mkataba uliopasishwa Geneva Uswisi, lakini licha ya kupita miaka kumi tangu isaini mkataba huo, utawala wake haukuchukua hatua yoyote ile ya kuasisi taasisi au jumuiya ambayo itatekeleza hati ya mkataba huo hapa Iran. ***

Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu

 

Miaka 119 iliyopita katika siku kama ya leo,  alizaliwa Walt Disney shakhsiya mashuhuri wa sekta ya filamu za watoto. Disney alizaliwa katika mji wa Chicago huko Marekani. Walt Disney alihitimu masomo katika Chuo Kikuu cha Havard na kutunukiwa shahada ya udaktari katika sayansi ya uchoraji na uchongaji (Fine Art). Disney alitoa mchango mkubwa katika kuimarisha sanaa ya filamu za katuni. Mara kadhaa alitunukiwa tuzo za Oscar katika uwanja huo wa kutengeneza filamu za katuni. Miongoni mwa kazi muhimu za Walt Disney ni Snow White, The Seven Dwarfs, Polar Bears. ***

Walt Disney

 

Siku kama ya leo miaka 40 iliyopita, alikufa shahidi rubani Ahmad Keshvari. Brigedia Ahmad Keshvari aliingia katika Jeshi la Anga la Iran mwaka 1351 Hijria Shamsia na kuhitimu mafunzo ya kuendesha helikopta. Baada ya ushindi wa Mapindizi ya Kiislamu nchini mwaka 1979 alitoa mchango mkubwa katika kupambana na makundi yaliyokuwa dhidi ya Mapinduzi katika maeneo ya magharibi mwa Iran na baadaye kidogo aliteuliwa kuwa kamanda wa Jeshi la Anga katika eneo la Ilam. Baada ya jeshi la Saddam Hussein kuvamia ardhi ya Iran, Brigedia Keshvari alikuwa mstari wa mbele kupambana na jeshi la adui na kulisababishia hasara kubwa ya nafsi na mali. Ahmad Keshvari aliuawa shahidi baada ya kukamilisha operesheni iliyokuwa na mafanikio akiwa njiani kurejea nchini.

Ahmad Keshvari

 

Miaka 30 iliyopita katika siku kama ya leo, alifariki dunia Manouchehr Jahan Beglu, profesa wa miziki ya kiasili ya Kiirani akiwa na umri wa mia 62. Profesa Jahan Beglu alizaliwa mwaka 1307 Hijria Shamsia Mwanamuziki huyo wa miziki ya kiasili alijifunza sanaa ya muziki kutoka kwa wasomi wakubwa wa tasnia hiyo na kisha akaelekea Austria na kupata shahada ya juu zaidi katika fani hiyo. Alirudi nchini na kuwasaidia wanafunzi wengi kufanya utafiti na kukuza tasnia hiyo.***

Manouchehr Jahan Beglu,

 

Katika siku kama ya leo miaka 24 iliyopita, mtayarishaji filamu mashuhuri wa Iran, Ali Hatami aliaga dunia. Baada ya kuhitimu masomo katika Chuo cha Sanaa hapa nchini, Hatami alijiunga na televisheni ya taifa na kujishughulisha na masuala ya filamu. Filamu zake nyingi ziliakisi mapenzi yake kwa utamaduni wa Iran. Miongoni mwa filamu hizo ni Sattarkhan, Sutedelan, Kamalul Mulk na Maadar.***

Ali Hatami

 

Siku kama ya leo miaka 7 iliyopita alifariki dunia shujaa wa mapambano ya ukombozi na kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela akiwa na umri wa miaka 95. Mandela alizaliwa mwaka 1918 na alitumia zaidi ya nusu ya umri wake akipambana na utawala wa kibaguzi nchini kwake. Utawala wa wazungu wabaguzi ulimfunga jela kwa kipindi cha miaka 27 hadi mfumo wa ubaguzi wa rangi ulipofutwa mwaka 1990. Mwaka 1994 wananchi wa Afrika Kusini walimchagua Nelson Mandela kuwa Rais wa kwanza mzalendo wa nchi hiyo. Baada ya kushika hatamu za uongozi, Mandela aliamiliana vyema na watala wa zamani wa mfumo wa ubaguzi wa rangi na hata wale waliomfunga jela na kumtesa. Mwenendo huo wa kusamehe ulizidisha umashuhuri na kupendwa shujaa huyo, na mwaka 1993 alitunukiwa tuzo ya amani ya Nobel. Kitabu mashuhuri zaidi cha shujaa huyo wa Afrika ni kile chenye kumbukumbu zake alichokipa jina la: "Njia Ndefu ya Kuelekea kwenye Uhuru". ***

Mzee Nelson Mandela

 

Na leo Disemba 5 ni Siku ya Kimataifa ya Wahisani ambao hujitolea kwa hali na mali kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu wengine. Kutenda wema na kufanya hisani ni suala ambalo halihusu, dini, taifa, wala kaumu makhsusi. Hata hivyo Uislamu ambayo ni dini ya mwisho ya Mwenyezi Mungu, umehimiza zaidi kutenda wema na hisani na kuwataja wahisani na watenda wema kwamba ni vipenzi vya Mwenyezi Mungu. Sehemu ya Aya ya 195 ya Suratul Baqara inasema: Na fanyeni wema. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wahisani.

Siku ya Kimataifa ya Wahisani na Wanaojitolea kwa ajili ya ustawi wa kiuchumi na kijamii