Ansarullah yatahadharisha kuhusu njama mpya za Marekani dhidi ya Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i101770-ansarullah_yatahadharisha_kuhusu_njama_mpya_za_marekani_dhidi_ya_yemen
Mwanachama wa ngazi ya juu wa harakati ya Ansarullah ya Yemen ametahadharisha kuhusu uwepo wa jeshi la Marekani nchini humo na kusema kuwa, lengo la hatua hiyo ni kuandaa mazingira mapya na kufanya njama hatari na endelevu dhidi ya taifa la Yemen.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 02, 2023 07:33 UTC
  • Ansarullah yatahadharisha kuhusu njama mpya za Marekani dhidi ya Yemen

Mwanachama wa ngazi ya juu wa harakati ya Ansarullah ya Yemen ametahadharisha kuhusu uwepo wa jeshi la Marekani nchini humo na kusema kuwa, lengo la hatua hiyo ni kuandaa mazingira mapya na kufanya njama hatari na endelevu dhidi ya taifa la Yemen.

Ali al-Kahhoum amesema kuwa, uwepo wa moja kwa moja wa jeshi la Marekani nchini Yemen unaonyesha dhamira ya njama za Washington na waitifaki wake na maandalizi ya kuanza awamu mpya ya mizozo ya kijeshi nchini Yemen.

Mwanachama huyu mwandamizi wa harakati ya Ansarullah ameendelea kusema kuwa: Majeshi ya Marekani yamepelekwa kwenye ardhi ya Yemen kwa lengo la kuweka uwiano kati ya Saudi Arabia na Imarati na kuzuia mapigano baina ya pande hizo mbili. Amesema madhumuni ya uwepo huo wa Marekani ni kuweka mazingira mapya katika nchi ya Yemen, kubakia siku zote nchini humo na kupanga njama hatari na endelevu dhidi ya taifa la Yemen.

Vita vya Saudia dhidi ya Yemen vilianza mwezi Machi mwaka 2015 kwa msaada na uungaji mkono wa Marekani, Imarati na nchi nyingine kadhaa, na vimesababisha uharibifu na hasara kubwa kwa taifa la Yemen.

Vita hivyo vimeua mamia ya maelfu ya Wayemeni na kusababisha hasara ya makumi ya mabilioni ya dola kwa uchumi wa nchi hiyo.