Kuchukuliwa hatua ndogo katika vita vya Ghaza ni muhimu lakini hakutoshi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i103814-kuchukuliwa_hatua_ndogo_katika_vita_vya_ghaza_ni_muhimu_lakini_hakutoshi
Licha ya kwamba mashambulizi ya mauaji ya umati ya utawala wa Kizayuni dhidi ya wakazi zaidi ya milioni mbili na laki tatu wa Ukanda wa Ghaza yameingia katika wiki ya tatu ambapo yamesababisha majeruhi na kuawa shahidi Wapalestina zaidi ya elfu 16 na zaidi ya wakazi wa Ghaza milioni moja kuhama makazi yao, lakini kuchukuliwa hatua kadhaa, japo ni madogo, huenda kukaandaa uwanja wa kudhibitiwa mapigano na kupunguzwa machungu ya wananchi wa Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 22, 2023 22:52 UTC
  • Kuchukuliwa hatua ndogo katika vita vya Ghaza ni muhimu lakini hakutoshi

Licha ya kwamba mashambulizi ya mauaji ya umati ya utawala wa Kizayuni dhidi ya wakazi zaidi ya milioni mbili na laki tatu wa Ukanda wa Ghaza yameingia katika wiki ya tatu ambapo yamesababisha majeruhi na kuawa shahidi Wapalestina zaidi ya elfu 16 na zaidi ya wakazi wa Ghaza milioni moja kuhama makazi yao, lakini kuchukuliwa hatua kadhaa, japo ni madogo, huenda kukaandaa uwanja wa kudhibitiwa mapigano na kupunguzwa machungu ya wananchi wa Palestina.

Kuachiwa huru kwa hiari wafungwa wawili wa Kimarekani wenye asili ya Israel na Hamas kwa upatanishi wa Qatar, kunaonyesha kuwa licha ya uungaji mkono mkubwa wa Marekani kwa utawala wa huo wa Kizayuni katika vita vya hivi sasa dhidi ya Ghaza ambavyo vinawalenga raia wa kawaida, lakini Hamas inaheshimu haki ya mateka na uhuru wao. Hii ni pamoja na kuwa zaidi ya 20 kati yao wamekufa kutokana na mashambulizi makali ya anga na makombora ya jeshi la Kizayuni kwenye maeneo ya Ghaza, na ni miili yao tu ndiyo inaweza kutumika katika mabadilishano ya mateka wa vita.

Hata hivyo, zaidi ya mateka 200 wa Israel, wakiwemo wanajeshi na raia bado wanashikiliwa na Hamas, ambao mustakabali wao utafahamika iwapo mashambulizi ya utawala wa Kizayuni yatasitishwa na kuwa na natija juhudi za upatanishi wa Qatar katika uwanja huo. Lakini iwapo utawala wa Kizayuni utaendelea na mashambulizi yake na kutaka kuanzisha operesheni ya nchi kavu dhidi ya Ghaza au kujaribu kutekeleza mpango mpya wa kuunda serikali ya muda huko Ghaza chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa, basi hakutakuwa na dhamana ya kulindwa roho ua kuachiliwa huru mateka waliosalia wa maghasibu wa Quds.

Uhalifu wa vita uliofanywa na Israel huko Ghaza

Hii ina maana kwamba uhuru wa mateka wa Israel uko mikononi mwa Netanyahu, kama ambavyo yeye mwenyewe ndiye anabeba dhima ya kukamatwa kwao.

Hii ni kwa sababu kwa upande mmoja, kuzingira kwa muda mrefu eneo la Ghaza, kumewafanya wanamapambano wa Hamas na wakazi wa Ukanda wa Ghaza kutekeleza operesheni iliyofana ya Kimbunga cha Al-Aqsa ili kujinasua kutoka mzingiro huo, na  kwa upande mwingine, kushughulizwa taasisi za kijasusi za utawala huo na siasa zao za chuki dhidi Iran kulizifanya kupuuza vitisho vya Hamas na kupata kishindo kikubwa zaidi kutoka kwa Hamas katika historia ya uhai wake.

Msafara wa misaada ya kibinadamu kwa ajili ya Ghaza

Ikiwa Netanyahu ataendelea na mashambulizi yake na kusababisha vifo vya mateka wa Israel, basi katika hali hiyo kesi nyingine itaongezwa kwenye morodha ya kesi zake zilizoko mahakamani, au mzozo mwingine na maandamano yataongezeka dhidi yake, kwa sababu kuna uwezekano kuwa atashtakiwa na familia za mateka kwa tuhuma za kufanya uzembe katika kuwaachia huru mateka wao.

Licha ya kuwa kutumwa misaada ya kwanza huko Ghaza, inaweza kuwa ni hatua moja mbele, lakini misaada hiyo haitoshi kwa vyovyote vile kwa sababu, kwanza mashambulizi ya utawala wa Kizayuni yangali yanaendelea na hakuna dhamana yoyote kwamba msafara wa misaada hiyo hautalengwa na Israel na pili ni kuwa, misaada hiyo haiwezi kukidhi mahitaji wala kufidia hasara kubwa iliyosabishwa na mashambulizi  makubwa ya anga na makombora ya utawala huo, hivyo kuna ulazima wa kuendelea kutolewa misaada hiyo kwa kiwango kikubwa na kwa muda mrefu.