Netanyahu akataa usitishaji vita wa siku tatu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i104508-netanyahu_akataa_usitishaji_vita_wa_siku_tatu
Waziri mkuu wa Israel amekataa ombi la Biden la kusitisha vita kwa siku tatu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 08, 2023 04:05 UTC
  • Netanyahu akataa usitishaji vita wa siku tatu

Waziri mkuu wa Israel amekataa ombi la Biden la kusitisha vita kwa siku tatu.

Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa Israel amekataa ombi la Rais Joe Biden wa Marekani la kusitisha mapigano kwa muda wa siku tatu.

Awali, tovuti ya habari ya Axios iliripoti kuwa Rais Joe Biden wa Marekani alikuwa amemtaka Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa Israel asitishe mapigano kwa siku tatu ili kutatua suala la mateka wanaoshikiliwa na wapiganaji wa Hamas.

Maafisa wa Marekani na Israel wameiambia Axios kwamba Biden amesema kusimamishwa vita kwa siku tatu kunaweza kusaidia kuachaliwa baadhi ya mateka walioko Gaza.

Rais Biden (kulia) na Netanyahu Waziri Mkuu wa Kizayuni

Afisa mmoja wa Marekani amesema katika kujibu habari hiyo kwamba pendekezo linalojadiliwa na Marekani, Israel na Qatar litajumuisha kuachiliwa na Hamas mateka 10 hadi 15 na muda huo wa siku tatu kusaidia kuthibitisha utambulisho na kutolewa orodha ya majina ya mateka wote wanaoshikiliwa na Hamas.

Ikulu ya White House awali ilisema kuwa Biden na Netanyahu walikuwa wamejadili uwezekano wa kusimamishwa vita kwa muda ili kuruhusu kuachiliwa mateka.

Harakati ya Muqawama ya Hamas 7 Oktoba ilifanya operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa  dhidi ya utawala wa kigaidi wa Kizayuni, nao utawala wa Kizayuni ukanzisha mashambulizi ya kila upande dhidi ya Ukanda wa Gaza, ambayo hadi sasa yamepelekea kuuawa shahidi Wapalestina elfu10,22, wakiwemo watoto 4,104

Kadhalika, watu 25,000 wamejeruhiwa katika mashambulizi yanayoendelea ya utawala wa Kizayuni, ambapo wengi wao ni watoto. Wizara ya Afya ya Palestina imesajili kesi 2,350 za watu waliopotea, ambapo karibu 1,300 ni watoto.