Jihad Islami: Wapigania ukombozi wa Palestina wameisababishia Israel hasara kubwa
Mrengo wa muqawama au wapigania ukombozi wa Kiisalmu wa Palestina wameusababishia utawala haramu wa Israel "hasara kubwa" licha ya kuwa "zana chache kijeshi."
Hayo yamedokezwa na mwanachama wa harakati ya muqawama ya Jihad Islami katika mahojiano maalumu na Press TV, ambapo amebainishwa kuwa, utawala wa Israel "umekiri kwa kiasi" kuwa kushindwa.
Ali Abu Shahin, mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Jihad ya Kiislam, alisema katika mahojiano maalum na Press TV kwamba utawala wa Israel " hauchapishi ripoti kamili kuhusu hasara zake vitani."
Kwa mujibu wa Abu Shahin, utawala wa Israel "unajitahidi" kutofichua hasara zake katika vita ili "kutovunja motisha ya wanajeshi wake na walowezi wa Kizayuni."
Amesema kadiri utawala wa Kizayuni wa Israel unavyozidisha mashambulio dhidi ya taifa la Palestina na ukanda wa Gaza, ndivyo hasara inavyozidi kuongezeka kwa utawala huo."
Kwingineko, Abu Shahin amepinga madai ya Israel kwamba harakati za kupigania ukombozi wa Palestina hutumia hospitali kama makao makuu ya operesheni.
Amesema utawala wa Kizayuni unaibua madai hayo yasiyo na msingi ili kuhalalisha mashambulizi yake katika vituo vya afya na misikiti katika eneo lililozingirwa la Gaza.
Mashambulio makali ya Israel kutoka angani, nchi kavu na baharini yanaendelea kuripotiwa katika sehemu kubwa ya Ukanda wa Gaza. Mashambulio hayo ya mara kwa mara yanasababisha vifo vya raia zaidi, kufurushwa na uharibifu wa miundombinu ya raia.
Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Gaza, tangu Oktoba 7 wakati utawala haramu wa Israel ulipoanzisha vita vya mauaji ya kimbari Gazam Wapalestina wasiopungua 29,092 wameuahwa shahidi katika eneo hilo na wengine 69,028 wamejeruhiwa. Aghalabu ya waliouawa na kujeruhiwa ni wanawake na watoto wasio na hatia.