Gazeti la Kizayuni: Wanajeshi wa Israel ni wezi wakubwa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i108658-gazeti_la_kizayuni_wanajeshi_wa_israel_ni_wezi_wakubwa
Gazeti moja la utawala wa Kizayuni limelazimika kukiri kuwa wanajeshi wa Israel ni waporaji na wezi wakubwa kutokana na kukithiri ujambazi na wizi wa majumbani wa wanajeshi hao katika maeneo mbalimbali ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghazza.
(last modified 2024-02-21T23:10:19+00:00 )
Feb 21, 2024 23:10 UTC
  • Gazeti la Kizayuni: Wanajeshi wa Israel ni wezi wakubwa

Gazeti moja la utawala wa Kizayuni limelazimika kukiri kuwa wanajeshi wa Israel ni waporaji na wezi wakubwa kutokana na kukithiri ujambazi na wizi wa majumbani wa wanajeshi hao katika maeneo mbalimbali ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghazza.

Televisheni ya al Alam imeripoti habari hiyo na kumnukuu Yagil Levy, mtaalamu wa masuala ya kijeshi wa Israel akiandika kwenye makala yake maalumu iliyochapishwa na gazeti la Kizayuni la Haaretz kwamba, wanajeshi wa Israel huwa wanafanya uporaji na wizi mkubwa wanapoingia kwenye nyumba za wakazi wa Ukanda wa Ghazza.

Ameandika, hata gazeti la Yedioth Ahronoth nalo limenukuu ushahidi wa daktari mmoja wa akiba na kuripoti kwamba, wanajeshi wa Israel wanapoingia kwenye nyumba za Wapalestina wanaiba kila kitu mpaka simu za mkononi, pikipiki na hata baskeli. Mwandishi huyo amehoji kwa kusema je, huu ni uadilifu?

Wanajeshi Wazayuni walafi na wasio na huruma, wanawaibia hata watu wanaoteseka kwa njaa kama hawa

 

Katika sehemu nyingine ya makala yake ameandika, mwanajeshi mmoja wa Israel amefikia hata kusambaza video kwenye mitandao ya kijamii akijifakharisha kwa kuiba jezi za wachezaji mpira wa timu za Palestina huko Ghaza. Video nyingine zinaonesha namna wanajeshi hao walafi wa Israel wanavyofakamia vyakula vya wakazi wa Ukanda wa Ghazza wanapoingia kwenye nyumba za raia hao wa Palestina.

Mwandishi huyo wa gazeti la Kizayuni la Haaretz ameongeza kuwa, ushahidi mwingi na mkubwa kiasi chote hicho unaootolewa kwa maandishi na matamshi na wanajeshi wa Israel, ni ushahidi wa jinsi wanajeshi hao walivyo waporaji na wezi wakubwa na hilo ni tatizo ambalo si dogo, lakini inavyoonekana jeshi la Israel halina nia kabisa ya kuzuia vitendo hivyo vya kijambazi na vya uporaji vya wanajeshi wake wa vyeo tofauti.