Walowezi wa Kizayuni wachoma moto mashamba ya Wapalestina huko Ramallah
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i113788-walowezi_wa_kizayuni_wachoma_moto_mashamba_ya_wapalestina_huko_ramallah
Walowezi wa Kizayuni ambao kwa miaka mingi wanakalia kwa mabavu ardhi za Wapalestina wameteketeza moto sehemu kubwa ya mashamba ya Wapalestina kaskazini mwa Ramallah.
(last modified 2024-07-07T04:36:17+00:00 )
Jul 07, 2024 04:36 UTC
  • Walowezi wa Kizayuni wachoma moto mashamba ya Wapalestina huko Ramallah

Walowezi wa Kizayuni ambao kwa miaka mingi wanakalia kwa mabavu ardhi za Wapalestina wameteketeza moto sehemu kubwa ya mashamba ya Wapalestina kaskazini mwa Ramallah.

Jumamosi, walowezi wa Kizayuni walishambulia kijiji cha "Tarmsaiya" kaskazini mwa Ramallah, kilichoko katikati ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuteketeza kwa moto sehemu kubwa ya mashamba ya Wapalestina.

Walowezi wa Kizayuni, baada ya kuvamia na kuharibu mashamba ya kilimo ya Wapalestina katika eneo la "Al-Taiba", lililoko magharibi mwa mji wa al-Khalil waliwafyatulia risasi na kuwajeruhi Wapalestina watano katika tukio hilo.

Walowezi wa Kizayuni wachoma moto nyumba na mashamba ya Wapalestina huko Ramallah

Huko "Umm Safa" kaskazini mwa Ramallah, mapigano yalitokea kati ya vikosi vya utawala katili wa Israel na vijana wa Kipalestina, ambapo wanajeshi wa Kizayuni waliwafyatulia Wapalestina risasi, mabomu ya sauti na gesi ya sumu.

Katika kukabiliana na jinai za kinyama zinazofanywa na jeshi la Kizayuni dhidi ya wananchi wa Palestina hususan watu wa Ukanda wa Gaza na wa mji wa Rafah, makundi ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina yaliharibu vifaru vinne vya Merkava vya jeshi la utawala wa Kizayuni.

Vikosi vya shahidi Ezzeddin al-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Palestina (Hamas) pia vimeua au kujeruhi baadhi ya askari hao vamizi kwa kulipua mabomu kwenye njia yao katika eneo la Al-Shuja'iyeh.

Watawala wa Tel Aviv walikiri hivi karibuni kuwa idadi ya wanajeshi wao waliouawa katika makabiliano na Wapalestina imefikia watu 674.

Wanasema idadi ya askari waliojeruhiwa tangu kuanza vita vya Gaza tarehe 7 Oktoba mwaka jana imefikia watu elfu 4 na 21.

Hii ni katika hali ambayo vyombo vya habari na wachambuzi wa mambo wanaichukulia idadi ya wahanga wa utawala wa Kizayuni kuwa kubwa zaidi kuliko hiyo iliyotangazwa kutokana na udhibiti mkali unafanywa na viongozi wa Kizayuni kuhusiana na habari za vita.