Mamilioni waandamana Yemen kuunga mkono Wapalestina wa Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i115326-mamilioni_waandamana_yemen_kuunga_mkono_wapalestina_wa_gaza
Mamilioni ya wananchi wa maeneo tofauti ya Yemen wameandamana na kusisitiza himaya na uungaji mkono wao kwa taifa la Palestina hususan wa Gaza.
(last modified 2024-08-17T03:44:49+00:00 )
Aug 17, 2024 03:44 UTC
  • Mamilioni waandamana Yemen kuunga mkono Wapalestina wa Gaza

Mamilioni ya wananchi wa maeneo tofauti ya Yemen wameandamana na kusisitiza himaya na uungaji mkono wao kwa taifa la Palestina hususan wa Gaza.

Mamilioni ya watu wa Yemen walioko Sana'a na mikoa mingine ya nchi hiyo jana walikusanyika katika medani kuu na kusisitiza kwa mara nyingine kwamba, wako pamoja na wakaazi wa Ukanda wa Gaza.

Washiriki wa maandamano hayo sambamba na kulaani kitendo cha kuvunjiwa heshima Msikiti wa Al-Aqswa na pia kutochukua hatua kwa baadhi ya nchi za Kiarabu na Kiislamu kwa jinai za utawala wa Kizayuni, wamepongeza mashambulizi ya maroketi ya muqawama wa Palestina katika kitovu cha Tel Aviv.

Waandamanaji wa Yemen wametangaza kuwa, hawataliacha taifa la Palestina peke yake na kwamba mashambulizi ya jeshi la Yemen dhidi ya adui Mzayuni hayatakoma kamwe.

Katika miezi ya hivii karibuni jeshi la Yemen limeendesha operesheni kadhaa za kiijeshi dhidi ya meli zinaoelekea Israel kama hatua ya kuunga mkono wakazi wa Gaza.

Operesheni za kijeshi za Yemen  dhidi ya meli zinazoelekea Israel zinafanyika kwa lengo la  kuwatetea Wapalestina

 

Yemen ilishatuma ilani rasmi kwa mashirika ya bima duniani na kutangaza kuwa  meli ambazo zote zinamilikiwa na watu binafsi  wanaohusishwa na Israel au mashirika ya utawala wa Israel; Meli zenye bendera ya Israel, au zile zinazomilikiwa na watu au mashirika ya Marekani au Uingereza, au kusafiri chini ya bendera za Marekani au Uingereza, zimepigwa marufuku kupita Bahari Nyekundu, Ghuba ya Aden na Bahari ya Arabia.

Operesheni hizo za kijeshi za Yemen ni katika kuwatetea Wapalestina ambao wanakabiliwa na hujuma ya utawala haramu wa Israel kwa himaya ya Marekani na Uingereza.