Utawala wa Kizayuni waendeleza jinai nchini Lebanon, Hizbullah yajibu jinai hizo
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i116712-utawala_wa_kizayuni_waendeleza_jinai_nchini_lebanon_hizbullah_yajibu_jinai_hizo
Utawala wa Kizayuni unaendelea kufanya jinai za kushambulia maeneo ya raia nchini Lebanon. Harakati ya Hizbullah nayo imeendelea kujibu jinai hizo kiasi kwamba shughuli za mji wa Haifa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, zimekwamishwa na mashambuizi ya makombora ya Hizbullah.
(last modified 2024-09-24T04:00:17+00:00 )
Sep 24, 2024 04:00 UTC
  • Utawala wa Kizayuni waendeleza jinai nchini Lebanon, Hizbullah yajibu jinai hizo

Utawala wa Kizayuni unaendelea kufanya jinai za kushambulia maeneo ya raia nchini Lebanon. Harakati ya Hizbullah nayo imeendelea kujibu jinai hizo kiasi kwamba shughuli za mji wa Haifa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, zimekwamishwa na mashambuizi ya makombora ya Hizbullah.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Mehr, utawala wa Kizayuni umeendelea kukanyaga sheria zote za kimataifa kwa kuingia bila ya ruhusa katika anga ya Lebanon na kufanya mashambulizi kwenye makazi ya raia ambapo kwa mujibu wa taarifa za karibuni kabisa, mamia ya raia wa Lebanon wameuawa na kujeruhiwa katika jinai hizo mpya za Israel.

Hizbullah ya Lebanon nayo imejibu mashambulio hayo kwa kuyapiga kwa makombora maeneo ya kijeshi ya utawala wa Kizayuni na kuyasababishia madhara makubwa.

Televisheni ya Al Mayadeen imeripoti kuwa, ndege za utawala wa Kizayuni zimeendelea kufanya mashambulizi katika maeneo ya raia huko Lebanon.

Katika upande mwingine vyombo vya habari vimesambaza picha zinazoonesha maeneo ya Wazayuni yaliyoshambuliwa na Hizbullah vikiwemo viwanja vya ndege vya kijeshi, viwanda vya zana za kijeshi na maeneo mengine ya Wazayuni.

Kutokana na mashambulizi makali ya Hizbullah ya Lebanon, viwanda vyote vya maeneo ya  kaskazini na kusni mwa Haifa vimesimamisha kazi kama ambavyo shughuli za kila siku za mji huo wa Wazayuni nazo zimekwama kikamilifu.