Droni ya Marekani yatunguliwa na Harakati ya Ansarullah ya Yemen
Ndege moja isiyo na rubani ya Marekani imetunguliwa kaskazini mwa Yemen leo Jumatatu asubuhi.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Iran Press, ndege hiyo isiyo na rubani ni aina ya MQ9 na imetunguliwa angani ikiwa katika mkoa wa Saada kaskazini mwa Yemen.
Kabla ya hapo wanajeshi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen tayari walikuwa wamefuatilia na kutungua ndege nyingine kadhaa za aina hiyokatika anga ya maeneo tofauti ya Yemen, hasa katika mkoa wa Marib. Ndege hiyo isiyo na rubani imeundwa kwa ajili ya kufanya operesheni za ujasusi za muda mrefu katika masafa ya juu.
Wananchi wa Yemen wanasisitiza kuwa wataendelea kuimarisha uwezo wao wa kiulinzi kwa ajili ya kukabiliana na uvamizi wa Marekani, Uingereza na vikosi vyote vya uvamizi na pia kuliunga mkono taifa madhulumu la Palestina huko Ukanda wa Gaza hadi kukomeshwa uvamizi wa utawala ghasibu wa Israel na vile vile mzingiro wa Wazayuni katika eneo hilo.