Wanajeshi wa Israel waendelea kupokea vipigo kutoka kwa wanamapambano wa Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i120818-wanajeshi_wa_israel_waendelea_kupokea_vipigo_kutoka_kwa_wanamapambano_wa_palestina
Kundi la Saraya al-Quds, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Jihad al Islami ya Palestina, limetangaza kwamba limefanikiwa kutoa kipigo kipya na kikali mno kwa wanajeshi makatili na vamizi wa Israel huko Ghaza.
(last modified 2024-12-30T23:21:52+00:00 )
Dec 30, 2024 23:21 UTC
  • Wanajeshi wa Israel waendelea kupokea vipigo kutoka kwa wanamapambano wa Palestina

Kundi la Saraya al-Quds, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Jihad al Islami ya Palestina, limetangaza kwamba limefanikiwa kutoa kipigo kipya na kikali mno kwa wanajeshi makatili na vamizi wa Israel huko Ghaza.

Katika taarifa yake hiyo, Saraya Al-Quds imesema kwamba, wanapambano mashujaa wa Jihadul Islami wamesambaratisha askari na zana za kijeshi za utawala wa Kizayuni katika kambi ya "Jabalia" ya kaskazini mwa Ghaza, kwa kufanya mashambulizi ya makombora na droni yaani ndege zisizo na rubani, wakati wanajeshi wa Israel walipokuwa wanafanya ujasusi na kujaribu kuudhibiti mji wa Ghaza. 

Vikosi vya Shahidi Omar Qasim pia vimeripoti kufanyika mashambulizi ya makombora kwenye kituo ambacho wanajeshi vamizi wa Israel walikuwa wamekusanyika wakiwa na zana zao za kijeshi, kwenye lango la kuingilia mji wa Salahuddin kusini mwa mji wa Rafah.

Taarifa hiyo aidha imesema kuwa, vikosi vya shahidi "Abu Ali Mustafa" vimeshambulia kituo cha operesheni cha adui Mzayuni katika eneo la Netsarim.

Wanamapambano wa Muqawama wa Palestina wameangamiza wanajeshi wengine wawili wa Israel katika shambulio jingine walilofanya katikati ya ukanda wa Ghaza.

Jeshi la Israel ambalo ni maarufu sana kwa kuchuja mno habari za vipigo linavyopata, kuhusu matukio ya hivi sasa limekiri kuwa afisa wa kikosi cha "Tasbar" chenye mfungamano na brigedi ya "Gafaati" amejeruhiwa katika mapigano makali na wanamapambano wa Palestina kaskazini mwa Ghaza.