HAMAS yatumia droni iliyoiteka kutoka kwa Israel kuwatwanga Wazayuni
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i120822-hamas_yatumia_droni_iliyoiteka_kutoka_kwa_israel_kuwatwanga_wazayuni
Brigedi za Izzudin Qassam, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS zimetangaza kuwa, zimetumia droni ziliyoiteka kutoka kwa wanajeshi wa Israel kuwashambulia wanajeshi hao vamizi na Wazayuni wenzao.
(last modified 2024-12-31T02:54:12+00:00 )
Dec 31, 2024 02:54 UTC
  • HAMAS yatumia droni iliyoiteka kutoka kwa Israel kuwatwanga Wazayuni

Brigedi za Izzudin Qassam, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS zimetangaza kuwa, zimetumia droni ziliyoiteka kutoka kwa wanajeshi wa Israel kuwashambulia wanajeshi hao vamizi na Wazayuni wenzao.

Hayo yameripoti ya shirika la habari la IRNA ambalo limeongeza kuwa, ndege moja isiyo na rubani ya utawala wa Kizayuni imetekwa na wanamapambano wa Palestina wa HAMAS na baada ya kugundua inavyofanya kazi, wanamuqawama wa Palestina wameitumia kushambulia wanajeshi wa Israel na vitongoji vya walowezi wa Kizayuni karibu na Ukanda wa Ghaza.

Hata msemaji wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel naye amekiri kutokea tukio hilo.

Kabla ya hapo pia, Brigedi za Izzudin Qassam, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Palestina HAMAS zilikuwa zimesambaza mkanda wa video unaoonesha jinsi wanamapambano hao walivyoteketeza kifaru cha Merkava cha jeshi vamizi la Israel.

Mkanda huo wa video umeonesha pia namna wanamapambano wa Palestina walivyotungua droni ya Evo Max ya jeshi la utawala wa Kizayuni katika kambi ya wakimbizi ya Jadid, kaskazini mwa eneo la al Naswirat la katikati mwa Ukanda wa Ghaza. 

Taarifa nyingine imesema kuwa, mwanamapambano mmoja wa HAMAS amefanikiwa kuangamiza idadi kadhaa ya wanajeshi vamizi wa Israel kwa bomu la mkono kaskazini mwa Ghaza na kuzidi kuthibitisha kuwa bado wanamapambano wa Palestina wako kwenye medani mbalimbali za mapambano dhidi ya wanajeshi makatili wa Israel.