Chombo cha Kizayuni: Hamas bado inadhibiti Ukanda wa Gaza
Chombo kimoja cha habari cha Kizayuni kimekiri kushindwa utawala huo katika vita dhidi ya Gaza na kutangaza kuwa, Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) bado inaudhibiti Ukanda wa Gaza.
Tovuti ya habari ya Walla imeripoti kuwa, Harakati ya Mapambano ya Kislamu ya Palestina (Hamas) imeweza kudumisha nguvu zake, na kwamba matukio yanayoshuhudiwa sasa yanaoonyesha kuwa harakati hiyo ipo kila mahali na inaudhibiti Ukanda wa Gaza licha ya kuwa vitani kwa muda mrefu.
Duru hiyo ya habari imeripoti kuwa, kusalia hai msemaji wa Brigedi za Shahidi "Izzedin al-Qassam", tawi la kijeshi la Hamas kuna maana ya kushindwa kwa taasisi mbili za kijeshi na kiusalama za utawala wa Kizayuni wa Israel.
Vyombo vingine vya habari vya Kizayuni pia vimeandika: Israel ilipoteza vita mnamo Oktoba 7, 2023 na baada ya hapo, kila hatua iliyochukuliwa ililenga kupunguza majeruhi na uharibifu wake.
Almog Cohen, mwakilishi wa Bunge la utawala wa Kizayuni wa Israel, Knesset huko nyuma alivitaja vikosi vyote vya jeshi la utawala huo kuwa vimeshindwa kuwajibika na kusema maafisa wake wanapaswa kufukuzwa jeshini na kurejea nyumbani.