Hamas 'yajiweka sawa' baada ya Israel kufanya shambulio la kinyama Jenin
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i121736-hamas_'yajiweka_sawa'_baada_ya_israel_kufanya_shambulio_la_kinyama_jenin
Wanajeshi wa Israel wamewauwa shahidi Wapalestina kumi na kuwajeruhi wengine 35 katika shambulio dhidi ya mji unaokaliwa kwa mabavu wa Jenin katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, na kupelekea Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas kutoa wito kwa vijana wa Kipalestina kujikusanya na kujiandaa kujibu uchokozi huo wa vikosi vamizi vya Wazayuni.
(last modified 2026-02-26T09:13:16+00:00 )
Jan 22, 2025 02:50 UTC
  • Hamas 'yajiweka sawa' baada ya Israel kufanya shambulio la kinyama Jenin

Wanajeshi wa Israel wamewauwa shahidi Wapalestina kumi na kuwajeruhi wengine 35 katika shambulio dhidi ya mji unaokaliwa kwa mabavu wa Jenin katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, na kupelekea Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas kutoa wito kwa vijana wa Kipalestina kujikusanya na kujiandaa kujibu uchokozi huo wa vikosi vamizi vya Wazayuni.

Vyombo vya habari vya Palestina vimeripoti kuwa, vikosi vya Kizayuni, vikisaidiwa na helikopta, vilivamia Jenin na kambi yake ya wakimbizi mapema jana Jumanne baaa ya mashambulizi kadhaa ya ndege zisizo na rubani.

Msemaji wa vikosi vya usalama vya Palestina, Anwar Rajab, amesema katika taarifa yake kwamba, vikosi vya Israel "vimewafyatulia risasi raia na vikosi vya usalama, na kusababisha majeraha kwa raia kadhaa na maafisa kadhaa wa usalama, ambao mmoja wao yuko katika hali mbaya".

Mashambulizi dhidi ya Jenin, ambapo majeshi ya utawala huo ghasibu yamefanya mashambulizi mengi na uvamizi mkubwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, yamekuja siku mbili tu baada ya kuanza utekelezwaji wa makubaliano ya usitishaji vita uliosubiriwa kwa muda mrefu kati ya Israel na Harakati ya Muqawama ya Palestina Hamas.

Hamas imesema katika taarifa kwamba, watu huko Gaza "wanaomboleza mashahidi wa Jenin ambao wameshambuliwa kwa risasi na mabomu ya wavamizi."

Katika hatua nyingine, Shirika la Ulinzi la Raia la Palestina la Gaza limeripoti kuwa, miili 137 ya raia waliouawa katika mashambulizi ya Israel imetolewa kwenye vifusi tangu kuanza kwa utekelezaji wa makubaliano ya usitishaji vita huko Rafah. Takriban miili 10,000 imefukiwa chini ya vifusi huko Gaza.