Carter: Kundi la Daesh linakaribia kupata silaha za kemikali
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i1522-carter_kundi_la_daesh_linakaribia_kupata_silaha_za_kemikali
Waziri wa Ulinzi wa Marekani amesema kuna uwezekano kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh likapata silaha za kemikali.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 19, 2016 04:13 UTC
  • Carter: Kundi la Daesh linakaribia kupata silaha za kemikali

Waziri wa Ulinzi wa Marekani amesema kuna uwezekano kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh likapata silaha za kemikali.

Ashton Carter amesema kuwa, Marekani inalifuatilia kwa karibu suala hilo lakini amesisitiza kwamba kuna uwezekano mkubwa wa jambo hilo kutokea.

Katika sehemu nyingine ya mazungumzo yake, Waziri wa Ulinzi wa Marekani amesema si ajabu kwamba magaidi hao wanazo silaha hizo. Amesema kikosi cha kimataifa kinachunguza suala hilo na ikibainika kwamba Daesh wanazo silaha za kemikali hatua za lazima zitachukuliwa kulizuia kundi hilo kutumia silaha hizo.

Indhari ya Ashton imetolewa katika hali ambayo Marekani ndiyo mfadhili mkubwa wa hali na mali wa makundi ya kigaidi katika nchi za Syria na Iraq na wachambuzi wanasema huenda hata silaha za kemikali zinazozungumziwa zimetoka Pentagon.