Magaidi watwangana wenyewe kwa wenyewe Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i22972-magaidi_watwangana_wenyewe_kwa_wenyewe_syria
Mapigano yamezuka baina ya magenge ya kigaidi ya ISIS (Daesh) na Jabhat al Nusra (Fat'h al Sham) katika kambi ya wakimbizi ya Yarmouk, kusini mwa Damascus, mji mkuu wa Syria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 06, 2017 23:49 UTC
  • Magaidi watwangana wenyewe kwa wenyewe Syria

Mapigano yamezuka baina ya magenge ya kigaidi ya ISIS (Daesh) na Jabhat al Nusra (Fat'h al Sham) katika kambi ya wakimbizi ya Yarmouk, kusini mwa Damascus, mji mkuu wa Syria.

Mwandishi wa Radio Tehran ameripoti habari hiyo na kuzinukuu kamati za uratibu wa makundi yenye silaha nchini Syria zikisema jana (Ijumaa) kuwa, mapigano yamezuka baina ya magenge ya kigaidi ya Daesh na Jabhat al Nusra kwenye kambi ya Yarmouk baada ya gaidi mmoja wa Jabhat al Nusra kujiripua kwa bomu katikati ya wanamgambo wa Daesh. Magaidi wanane wa ISIS wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa kwenye shambulio hilo.

Kwa upande wake, televisheni ya al Alam imeripoti habari ya kutokea mapigano baina ya makundi yenye silaha na wanamgambo wa Daesh katika eneo la al Qalamun, mashariki mwa Damascus na kupelekea kuuawa na kujeruhiwa wanamgambo kadhaa wa ISIS.

 

Wakati huo huo, duru za habari za Syria zilitangaza jana (Ijumaa) kuwa, Yunus Shoaib, maarufu kwa jina la Abu Hasan, mkuu wa genge la kigaidi la Jabhat al Nusra ameangamizwa katika mkoa wa Idlib, kaskazini magharibi mwa Syria.

Kesi za magaidi kushambuliana wao kwa wazo zimekuwa zikiripotiwa sana hususan wakati magenge ya kigaidi yanapozidiwa nguvu na jeshi la serikali ya Syria na waitifaki wake.