Jan 15, 2017 07:17 UTC
  • Maandaano ya kulaani ufisadi wa Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa israel mjini Tel Aviv
    Maandaano ya kulaani ufisadi wa Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa israel mjini Tel Aviv

Mamia ya wakazi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamefanya maandamano ya kulaani ufisadi wa kifedha wa viongozi wa utawala huo hususan Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel, mjini Tel Aviv.

Mtandao wa habari wa Quds Net umetangaza habari hiyo leo na kusema kuwa, mamia ya wakazi wa utawala wa Kizayuni jana usiku walikusanyika kwenye majengo ya Wizara ya Vita ya utawala huo na sambamba na kutaka Benjamin Netanyahu afutiwe kinga ya kutoshtakiwa, walisisitizia wajibu wa kupandishwa kizimbani haraka waziri mkuu huyo wa utawala wa Kizayuni.

Wakati huo huo gazeti la Kizayuni la Haaretz limeashiria kuwa maandamano hayo yameitishwa na muungano wa Wazayuni wa vyama vya Meretz na Leba na kwamba uchunguzi kuhusu ufisadi wa kifedha uliofanywa na Benjamin Netanyahu, umeanza. Kwa mujibu wa gazeti hilo, ufisadi huo wa kifedha wa Waziri Mkuu wa Israel ndiyo sababu kuu ya kufanyika maandamano hayo.

Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel

 

Naye mwandishi wa Kanali ya Pili ya televisheni ya Israel ameripoti kuwa, Benjamin Netanyahu na Arnon Mozes, mhariri mkuu wa gezeti la Kizayuni la Yediot Ahronot hivi sasa wanawasaka waandishi wa habari ili kuwashinikiza wasifuatilie suala la kuhusika Netanyahu kwenye kashfa hiyo kubwa.

Tarehe pili mwezi huu wa Januari, jeshi la polisi la utawala wa Kizayuni wa Israel lilimtuhumu Benjamin Netanyahu kuwa amefanya ufisadi wa fedha na kupokea mali kinyume cha sheria.

Viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameoza kwa ufisadi wa kila namna ukiwemo ufisadi wa ngono, wa fedha na kashfa nyingine nyingi za kimaadili. Mikono ya viongozi hao wa utawala wa Kizayuni wa Israel aidha imejaa damu za watu wasio na hatia hususan Wapalestina.

Tags