Utawala wa Kizayuni waidhinisha ujenzi wa nyumba mpya za walowezi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i35940-utawala_wa_kizayuni_waidhinisha_ujenzi_wa_nyumba_mpya_za_walowezi
Baraza la Mawaziri wa utawala wa Kizayuni limeidhinisha kujengwa nyumba mpya kwa ajili ya walowezi wa Kizayuni katika ardhi walizoporwa Wapalestina kwenye mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 25, 2017 12:01 UTC
  • Utawala wa Kizayuni waidhinisha ujenzi wa nyumba mpya za walowezi

Baraza la Mawaziri wa utawala wa Kizayuni limeidhinisha kujengwa nyumba mpya kwa ajili ya walowezi wa Kizayuni katika ardhi walizoporwa Wapalestina kwenye mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.

Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni leo ameafiki kujengwa nyumba mpya 176 za walowezi wa Kizayuni ndani ya eneo moja la makazi la raia wa Palestina huko Quds. 

Israel inaendeleza ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika hali ambayo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 23 Disemba mwaka jana lililipigia kura ya ndio azimio la umoja huo linalosisitiza kukomeshwa ujenzi wa vitongoji hivyo unaofanywa na utawala wa Kizayuni katika ardhi wanazoporwa Wapalestina. 

Viongozi wapenda vita wa Israel kila uchao wamekuwa wakizungumzia mipango mipya ya kujenga nyumba mpya za walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina tangu alipoingia katika ikulu ya Marekani (White House) Rais Donald Trump  na kutangaza uungaji mkono wake wa pande zote kwa utawala huo haramu. Katika upande mwingine, wanajeshi vamizi wa Kizayuni kwa mara 120 sasa wamekivamia na kufanya uharibifu katika kijiji cha al Araqiib kwenye ardhi zilizokaliwa kwa mabavu na Israel mwaka 1948. 

Wanawake wa Kipalestina wakiwa wamekimbilia makaburini katika kijiji cha al Araqiib baada ya wanajeshi wa Israel kukivamia kijiji hicho