Feb 01, 2018 07:55 UTC
  • Kibla cha Kwanza cha Waislamu kinachokaliwa kwa mabavu na Wazayuni
    Kibla cha Kwanza cha Waislamu kinachokaliwa kwa mabavu na Wazayuni

Sayyid Ali Fadhlullah, Imam wa Sala ya Ijumaa ya Beirut Lebanon na Sheikh Maher Hamoud, Mkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Maulamaa wa Muqawama wamesisitizia wajibu wa kuungana ulimwengu wa Kiislamu na wa Kiarabu katika kukabiliana na uadui wa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Sisitizo hilo limetolewa na shakhsia hao wawili wakati walipoonana na kufanya mazungumzo katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut, jana Jumatano. Wamegusia namna Israel na watu wenye fikra za Kizayuni kama rais wa Marekani, Donald Trump wanavyofanya njama dhidi ya Palestina na kuutaka umma wa Kiislamu kuwa macho na Waislamu kubakia katika njia sahihi ya kukabiliana na maadui wao wa pamoja badala ya kuzozana wao kwa wao. 

Wapenda haki wote duniani wana wajibu wa kupambana na Wazayuni makatili wasio na chembe ya ubinadamu

 

Imam wa Sala ya Ijumaa ya Beirut pia amesisitiza kwamba, umoja na mshikamano wa Kiislamu ndiyo stratijia pekee ya kuweza kuwasaidia Wapalestina na kuunga mkono muqawama. Amesema, Waislamu kote ulimwengu wanapaswa kusimama kidete kupambana na njama za rais wa Marekani Donald Trump za kutaka kuifuta kabisa kadhia ya Palestina kupitia kuitangaza Quds kuwa eti mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kwa upande wake, Sheikh Maher Mahmoud, Mkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Maulamaa wa Muqawama amesema, umoja huo daima umekuwa ukifanya juhudi za kulinda umoja wa Lebanon, wa Waarabu na wa Waislamu sambamba na kuulinda muqawama mbele ya adui Mzayuni. 

Tags