Silaha za Israel zapatikana katika ngome za ISIS (Daesh) Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i40957-silaha_za_israel_zapatikana_katika_ngome_za_isis_(daesh)_syria
Vyombo vya habari nchini Syria vimerusha kanda ya video inayoonyesha silaha zilizotengenezewa Israel, katika maeneo yaliyokombolewa hivi karibuni kutoka kwenye makucha ya kundi la kigaidi la Daesh (ISIS), mkoani Dayr al-Zawr.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 27, 2018 22:02 UTC
  • Silaha za Israel zapatikana katika ngome za ISIS (Daesh) Syria

Vyombo vya habari nchini Syria vimerusha kanda ya video inayoonyesha silaha zilizotengenezewa Israel, katika maeneo yaliyokombolewa hivi karibuni kutoka kwenye makucha ya kundi la kigaidi la Daesh (ISIS), mkoani Dayr al-Zawr.

Video hiyo mpya imeonyesha shehena za silaha zenye nambari za usajili za utawala wa Kizayuni, yakiwemo maroketi, maguruneti na vifaru  zilizonaswa na wanajeshi wa Syria katika miji ya Bukamal na Mayadin.

Kadhalika askari wa Syria wamegundua kituo cha kuzalisha mada za milipuko kilichokuwa kimesheheni kemikali mbali mbali zisizojulikana, katika moja ya ngome za zamani za Daesh mkoani Dayr al-Zawr. 

Silaha za Israel zilizokuwa zikitumiwa na ISIS Syria

Hii ni katika hali ambayo, siku chache zilizopita, televisheni ya CNN ilitangaza kuwa, silaha ambazo Marekani imeyapatia magenge ya kigaidi huko Syria hivi sasa zinapigwa mnada katika kurasa za Intraneti za magaidi hao.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, silaha ambazo Marekani iliyapa makundi yanayodaiwa kuwa na misimamo ya wastani kwa ajili ya kuipiga vita serikali halali ya Syria zimeingia mikononi mwa magenge ya kigaidi.