Rais Assad: Wanajeshi wa Marekani na Uingereza ni wavamizi nchini Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i45648-rais_assad_wanajeshi_wa_marekani_na_uingereza_ni_wavamizi_nchini_syria
Rais Bashar al Assad wa Syria amesema kuwa, madola ya Magharibi hayawezi kuiainishia nchi hiyo mustakbali wake na kusisitiza kuwa, wanajeshi wa Uingereza na Marekani walioko nchini humo ni wavamizi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 10, 2018 03:22 UTC
  • Rais Assad: Wanajeshi wa Marekani na Uingereza ni wavamizi nchini Syria

Rais Bashar al Assad wa Syria amesema kuwa, madola ya Magharibi hayawezi kuiainishia nchi hiyo mustakbali wake na kusisitiza kuwa, wanajeshi wa Uingereza na Marekani walioko nchini humo ni wavamizi.

Marekani na Uingereza zimetuma wanajeshi wao vamizi kinyume cha sheria nchini Syria kwa madai ya eti kupambana na ugaidi.

Nchi hizo za kibeberu zimetuma wanajeshi wao vamizi nchini Syria kwa madai ya kupambana na ugaidi katika hali ambayo kwa mujibu wa ripoti rasmi, Marekani na Uingereza ndio waanzilishi na waungaji mkono wakuu wa magenge ya kigaidi katika eneo hili ikiwemo Syria.

Wanajeshi wa Uingereza nchini Syria

 

Katika mahojiano aliyofanyiwa na gazeti la The Mail on Sunday la nchini Uingereza, Rais Bashar al Assad wa Syria amesema, Uingereza, Marekani na Ufaransa zilishirikiana kufanya mashambulizi ya kijeshi nchini humo kwa madai ya uongo ya kutumika silaha za kemikali katika eneo la Douma, karibu na mji mkuu Damascus.

Mhimili huo wa pande tatu wa shari yaani Marekani, Ufaransa na Uingereza zilifanya mashambulizi hayo tarehe 14 Aprili 2018, wiki moja baada ya kuenezwa madai ya uongo ya kutumika silaha za kemikali katika eneo la Douma, huko Ghouta Mashariki, na nchi hizo za kibeberu za Magharibi zilivurumisha makombora zaidi ya 100 katika maeneo tofauti ya Syria.

Baadaye lakini ilithibitika kuwa hakuna shambulizi kama hilo la kemikali lililofanyika huko Syria na kwamba mashambulizi hayo ya kinyama ya Marekani, Ufaransa na Uingereza yalifanyika tu kwa ajili ya kuyaunga mkono magenge ya kigaidi yaliyoelemewa na mashambulizi ya jeshi la Syria.