Syria yaikosoa Marekani kwa kuwasaidia wapiganaji wa Daesh
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i46368-syria_yaikosoa_marekani_kwa_kuwasaidia_wapiganaji_wa_daesh
Mwakilishi wa kudumu wa Syria katika Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine tena ameikosoa Marekani kwa kuwasaidia kwa silaha na fedha wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 26, 2018 21:43 UTC
  • Syria yaikosoa Marekani kwa kuwasaidia wapiganaji wa Daesh

Mwakilishi wa kudumu wa Syria katika Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine tena ameikosoa Marekani kwa kuwasaidia kwa silaha na fedha wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh.

Bashar al Ja'fari amekiambia kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichokutana kujadili hali ya Mashariki ya Kati kwamba: Marekani inawasaidia kwa silaha wapiganaji wa kundi la Daesh ili waendelee kushambulia jeshi la Syria.

Al Ja'fari ameongeza kuwa, Marekani inaendelea kuwapatia mafunzo watu wanaobeba silaha na magaidi katika vituo 19 zinavyokaliwa kwa mabavu ndani ya ardhi ya Syria. 

Mwakilishi wa kudumu wa Syria katika Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa, vilevile Marekani inawapatia silaha, nishati, chakula na misaada ya aina nyingine magaidi katika kambi zake 22 za kijeshi nje ya Syria.

Nyaraka zilizofichuliwa hivi karibuni katika maeneo yaliyokombolewa nchini Syria kutoka kwenye makucha ya makundi ya kigaidi zinaonesha kuwa, Marekani ingali inayasaidia kwa hali na mali makundi hayo hatari. 

Wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh

Kwa mfano tu imeripoti kuwa, ndege za kivita za muungano unaoongozwa na Marekani zimewasafarisha makamanda wawili wa kundi la kigaidi la Daesh kutoka eneo la Tuimin hadi katika kituo cha Marekani kilichoko katika mji wa al Shaddadah mkoani Hasakah nchini Syria. 

Nchi hiyo ilitumbukia katika machafuko na mgogoro wa ndani mwaka 2011 baada ya makundi ya kigaidi likiwemo la Daesh kuvamia ardhi ya Syria yakisaidiwa kwa hali na mali na Saudi Arabia, Marekani, Israel na waitifaki wao.