Syria yafichua kuwa Marekani inawapatia magaidi mafunzo na silaha huko Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i46378-syria_yafichua_kuwa_marekani_inawapatia_magaidi_mafunzo_na_silaha_huko_syria
Duru za habari zimearifu kuhusu awamu mpya ya misaada ya Marekani kwa magaidi huko Syria katika kipindi hiki cha utawala wa Donald Trump.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 27, 2018 03:20 UTC
  • Syria yafichua kuwa Marekani inawapatia magaidi mafunzo na silaha huko Syria

Duru za habari zimearifu kuhusu awamu mpya ya misaada ya Marekani kwa magaidi huko Syria katika kipindi hiki cha utawala wa Donald Trump.

Wakati huo huo Mwakilishi wa Kudumu wa Syria katika Umoja wa Mataifa, Bashar al Ja'afar pia amefichua kuwa Marekani kwa kiasi kikubwa inawapatia mafunzo magaidi katika vituo 19 vinavyoshikliliwa na magaidi hao ndani ya Syria na wakati huo huo inawapa silaha na zana za kijeshi.  

 

Bashar al Ja'afar, mwakilishi wa Kudumu wa Syria katika UN

Jarida la The American Conservative limeandika kuwa licha ya ahadi iliyotolewa miezi kadhaa iliyopita na Donald Trump ya kuondoka Syria na kuwarejesha Marekani wanajeshi wa nchi hiyo, ripoti zinaonesha kuwa, Marekani na waitifaki wake zikiwemo Uingereza, Ufaransa, Israel, Jordan na baadhi ya nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi zinaendelea kuyapa misaada makundi ya kigaidi huko Syria. 

Muungano eti wa kupambana na ugaidi unaoongozwa na Marekani sasa umekuwa taasisi inayoanzisha na kuyasaidia makundi ya kigaidi katika eneo la Mashariki ya Kati. Lengo la harakati za muungano huo wa Kimarekani ni kudhoofisha nchi hiyo na kuharibu kikamilifu miundombinu yake na vilevile kuzusha hofu na wahka miongoni mwa wananchi wa Syria ili kuwafanya wasitishe mapambano yao dhidi ya magaidi. Hata hivyo wananchi na jeshi la Syria limeendelea kusimama kidete na limefanikiwa kukomboa maeneo mengi ya nchi hiyo yaliyokuwa yakikaliwa kwa mabavu na makundi ya kigaidi hususan lile la Daesh. Mafanikio haya yamewatia wasiwasi mkubwa waungaji mkono wa makundi haya hususan Marekani na Israel. Ni kwa sababu hiyo ndipo Marekani ikaanzisha harakati mpya ya kuwapa mafunzo na silaha wanachama wa makundi hayo ya kigaidi na kuendelea kuwepo kijeshi nchini humo. Hii ni pamoja na kuwa kuwepo wanajeshi wa Marekani katika ardhi ya Syria bila ya idhini ya serikali ya nchi hiyo au Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ni sawa kabisa na uvamizi wa kijeshi. 

Kwa sasa inaonekana kuwa njama hizo zote za Marekani na waitifaki wake zimegonga mwamba licha ya kuwepo huko Syria kwa miaka kadhaa na licha ya misaada ya hali na mali inayoendelea kutolewa kwa makundi ya kigaidi nchini humo. Njama hizo zimeshindwa na kufeli huku Marekani, Israel, Uingereza na vibaraka wao wa Kiarabu wakiendelea kukusanya pamoja mabaki ya wapiganaji wa makundi kama Daesh, Jabhat al Nusra, Ahrarul Sham; na kadhalika na kuwapa mafunzo na silaha wakiwa na stratijia mpya. 

Magaidi wa Jabhatul Nusra huko Syria 

Mwandishi na mwanaharakati wa masuala ya kijamii wa Marekani Michael Springmann anasema: Njia ya kukomesha kabisa ugaidi na kundi la Daesh ni kusimamisha upelekeaji wa misaada kama ya pesa, silaha na kuwapa mafunzo wanachama wa makundi hayo.

Mgogoro wa Syria umeonesha kwamba, harakati hizo ni njama ya nchi za kigeni zikiongozwa na Marekani zinazotumia makundi ya kuigaidi kwa ajili ya kufikia malengo yao. Hata hivyo kusimama kidete kwa jeshi na wananchi wa Syria kumekwamisha njama za maadui hao.