Jul 01, 2018 13:58 UTC
  • Utawala wa Aal Khalifa unaratibu mipango ya kuwauwa viongozi wanamapinduzi

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya al Amal ya Bahrain ameeleza kuwa utawala wa Aal Khalifa unaratibu mipango ya kuwauwa viongozi wanamapinduzi wa nchi hiyo.

Sheikh Abdullah Saleh ameongeza kuwa utawala wa Bahrain siku zote umekuwa ukitekeleza vitendo visivyo vya kibinadamu dhidi ya viongozi wanamapinduzi wa nchi hiyo wakiwemo Sheikh Issa Qassim mwanazuoni mtajika wa nchi hiyo, Nabil Rajab mwanaharakati wa haki za binadamu na makumi ya wanazuoni wengine wa nchi hiyo.

Sheikh Issa Qassim, mwanazuoni mtajika wa Bahrain ambaye amehukumiwa kifungo cha nyumbani 

Naibu Katibu Mkuu wa harakati ya Kiislamu ya al Amal ya nchini Bahrain amesisitiza kuwa kuwatesa na kuwabugudhi raia wa Bahrain wakiwemo maulamaa wa kidini wa nchi hiyo ni suala lililowekwa katika ajenda ya kazi ya viongozi wa utawala wa Aal Khalifa; na kwamba wafungwa nchini humo wanaaga dunia taratibu kufuatia hatua ya utawala wa Bahrain ya kuakhirisha matibabu na kufikishwa hospitalini raia hao.  

Sheikh Abdullah Saleh aidha ameashiria nafasi ya utawala wa Aal Khalifa katika kuhuishwa uhusiano kati ya tawala za Kiarabu na utawala wa Kizayuni na kueleza kuwa: Bahrain ni nchi pekee katika eneo la Ghuba ya Uajemi ambayo viongozi wake kama Mfalme, Mrithi wa Kiti cha Ufalme na Waziri wa Mambo ya Nje wameshakutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa utawala wa Kizayuni. Sheikh Saleh ameongeza kuwa viongozi wa Bahrain wanaalika waziwazi nchini humo jumbe za utawala wa Kizayuni au kutuma jumbe tofauti huko Israel. 

 

Tags