Nov 03, 2018 08:00 UTC
  • Bin Salman akutana na Wakristo wanaounga mkono utawala haramu wa Kizayuni

Mohammad Bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia, amekutana na kufanya mazungumzo na wajumbe wa tume ya Kimarekani inayounga mkono utawala haramu wa Kizayuni, ambao walikuwa wamefanya safari nchini Saudia.

Tume hiyo ilikuwa imewashirikisha wajumbe wa zamani wa kogresi ya Marekani na viongozi wa asasi kadhaa za nchini Marekani zinazoiunga mkono Israel kama vile taasisi ya 'Jerusalem Prayer Team.' Aidha wanachama wa tume hiyo ya Kimarekani wamekutana na Adel al-Jubeir, Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia. Hatua hiyo ya Mohammad Bin Salman ya kukutana na tume hiyo ya Wakristo wenye misimamo mikali wanaouunga mkono utawala katili wa Kizayuni na ndani ya ardhi ya Saudia, inaonyesha juhudi zake kwa ajili ya kudumisha uhusiano mwema na Tel Aviv katika mazingira ya sasa. Kabla ya hapo pia, Mrithi huyo wa Kiti cha Ufalme wa Saudia na akifanya mahojiano na jarida moja la Kimarekani la Atlantic alidai kwamba, Waisrael wanayo haki ya kuwa na ardhi yao.

Pande tatu za Marekani, Israel na Saudia ambazo ni washirika wakubwa

Kuongezeka mwenendo wa kufanya uhusiano mwema rasmi kati ya utawala haramu wa Kizayuni na Saudi Arabia, kunajiri katika hali ambayo kabla ya hapo tume ya maulama ya nchi hiyo ilitangaza kwamba, hatua hiyo ni sawa na kuyafanyia hiyana matukufu ya Palestina.

Tags