Mazungumzo ya Dakta Zarif na Rais Bashar al-Assad wa Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i52888-mazungumzo_ya_dakta_zarif_na_rais_bashar_al_assad_wa_syria
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambaye yuko safarini nchini Syria, leo amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Bashar al-Assad wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Apr 16, 2019 14:41 UTC
  • Mazungumzo ya Dakta Zarif na Rais Bashar al-Assad wa Syria

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambaye yuko safarini nchini Syria, leo amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Bashar al-Assad wa nchi hiyo.

Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wawili wamezungumzia masuala ya pande mbili, ya kieneo na kimataifa sambamba na kujadili matukio ya hivi karibuni kabisa katika eneo la Mashariki ya Kati.

Kadhalika Dakta Muhammad Javad Zarif na Rais wa Syria wamejadili mambo yaliyoafikiwa na pande mbili katika safari ya hivi karibuni ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran huko nchini Syria.

Aidha Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akiwa mjini Damascus amekutana na kufanya mazungumzo na Walid al-Muallim, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Syria na kusema kuwa, kusimama kidete serikali na wananchi wa Syria dhidi ya ugaidi kumeliokoa eneo la Mashariki ya Kati na hatari na njama kubwa.

Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran na Syria

Kwa upande wake, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Syria ameashiria ushirikiano wa pande mbili katika miaka ya hivi karibuni na kubainisha kwamba, ushirikiano huu umezifanya nchi mbili hizi kusambaratisha njama kubwa na hivyo kuna haja ya kuendelezwa kwake katika nyanja mbalimbali.

Dakta Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo aliwasili Damascus mji mkuu wa Syria kwa shabaha ya kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa nchi hiyo.