Saeb Erekat: Siasa za Marekani katika mkutano wa Bahrain zitafeli
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i54252-saeb_erekat_siasa_za_marekani_katika_mkutano_wa_bahrain_zitafeli
Katibu wa Chama cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Saeb Erekat amesema kuwa siasa za Marekani katika kikao cha uchumi kinachosimamiwa na Washington nchini Bahrain, zitashindwa tu.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 21, 2019 07:23 UTC
  • Saeb Erekat: Siasa za Marekani katika mkutano wa Bahrain zitafeli

Katibu wa Chama cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Saeb Erekat amesema kuwa siasa za Marekani katika kikao cha uchumi kinachosimamiwa na Washington nchini Bahrain, zitashindwa tu.

Sambamba na kulaani siasa za Washington dhidi ya matukufu ya taifa la Palestina amesema kuwa, sehemu ya uchumi ya kikao hicho cha Bahrain kuhusiana na kadhia ya Palestina ni juhudi kwa ajili ya kubadili msingi wa 'fedha mkabala wa usalama' badala ya 'ardhi mkabala wa amani.' Kwa mujibu wa katibu huyo wa Palestina (PLO) mpango wa Muamala wa Karne wa Marekani ni 'kustawisha na kuendelezwa vitongozi vya walowezi wa Kizayuni' katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavuu za Palestina na kuongeza kwamba, hatua za Marekani kama zile za kuutambua mji wa Quds kuwa mji mkuu wa utawala huo wa Kizayuni, kuhamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv kwenda mji huo, kuutaja kuwa wa kisheria ujenzi wa vitongoji vya walowezi na kusambaratisha juhudi za kuundwa taifa la Palestina, ni sehemu ya mpango huo wa Kimarekani.

Saeb Erekat, Katibu wa Chama cha Ukombozi wa Palestina (PLO)

Hii ni katika hali ambayo Ismail Haniyeh, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Palestina HAMAS pia ameutaja mkutano huo wa Bahrain kuwa sehemu ya njama za Marekani na Israel za kusambaratisha matukufu ya Palestina na kuitaka serikali ya Manama kuachana na mpango wake wa kuwa mwenyeji wa mkutano huo. Mkutano huo wa hatua ya kwanza kwa ajili ya kutekelezwa mpango wa Muamala wa Karne umepangwa kufanyika tarehe 25 na 26 za mwezi huu huko Manama, mji mkuu wa Bahrain.