Sayyid Ammar al Hakim: Quds ni utambulisho wa Waislamu wote
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i58888-sayyid_ammar_al_hakim_quds_ni_utambulisho_wa_waislamu_wote
Mkuu wa Baraza Kuu la Kiislamu la Iraq amelaani njama mpya za rais wa Marekani Donald Trump za "Muamala wa Karne" ambazo zinalenga kuwapora Waislamu maeneo yao matakatifu hasa Kibla chao cha Kwanza yaani Msikiti wa al Aqsa na kusisitiza kuwa, rais wa Marekani anapaswa kutambua kuwa Quds ni utambulisho wa Waislamu wote na watasimama kidete kulilinda eneo lao hilo takatifu kwa nguvu zao zote.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Feb 02, 2020 02:42 UTC
  • Sayyid Ammar al Hakim: Quds ni utambulisho wa Waislamu wote

Mkuu wa Baraza Kuu la Kiislamu la Iraq amelaani njama mpya za rais wa Marekani Donald Trump za "Muamala wa Karne" ambazo zinalenga kuwapora Waislamu maeneo yao matakatifu hasa Kibla chao cha Kwanza yaani Msikiti wa al Aqsa na kusisitiza kuwa, rais wa Marekani anapaswa kutambua kuwa Quds ni utambulisho wa Waislamu wote na watasimama kidete kulilinda eneo lao hilo takatifu kwa nguvu zao zote.

Katika taarifa yake ya jana Jumamosi, Sayyid Ammar al Hakim alisema, Quds ni kadhia ya kibinadamu, Kiislamu na Kiarabu na inamuhusu kila Muislamu na kila mpenda haki duniani, hivyo njama zozote za kujaribu kuwapora Waislamu Kibla chao hicho cha Kwanza au kulipiga mnada eneo hilo kwa sababu ya uchaguzi, ni jambo lisilokubalika kabisa.

Amesisitiza kuwa, muamala huo muovu kabisa hauna thamani yoyote na kwamba, taifa la Palestina na mpenda haki yeyote duniani kama hawezi kukubaliana nao.

Muamala wa Karne

Mkuu huyo wa Baraza Kuu la Kiislamu la Iraq aidha amelitaka Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na taasisi nyingine za umoja huo zishirikiane na Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kupambana na njama hizo za kukanyaga waziwazi haki za Wapalestina na za Waislamu.

Wananchi wa nchi mbalimbali duniani juzi Ijumaa walifanya maandamano makubwa kulaani njama mpya za Marekani za kutaka kuwapora Wapalestina na Waislamu kiujumla maeneo yao matakatifu. 

Mpango wa Muamala wa Karne uliopendekezwa na Marekani unajumuisha kukabidhiwa kikamilifu Israel mji mtakatifu wa Quds wenye Kibla cha Kwanza cha Waislamu yaani Msikiti wa al Aqsa, vitongoji vilivyoko katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan vyote ipewe Israel, Wapalestina wasiwe na haki ya kurejea kwenye ardhi za mababu zao na makundi ya muqawama wa Palestina yapokonywe silaha ili kusiwe na jambo lolote linalohatarisha usalama wa utawala wa Kizayuni wa Israel.