HAMAS: Njia pekee ya kuzikomboa ardhi za Palestina ni mapambano
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i60070-hamas_njia_pekee_ya_kuzikomboa_ardhi_za_palestina_ni_mapambano
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imesisitiza tena kwamba, njia pekee ya kuzikomboa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni maghasibu ni mapambano.
(last modified 2026-08-14T10:24:44+00:00 )
Mar 30, 2020 23:16 UTC
  • HAMAS: Njia pekee ya kuzikomboa ardhi za Palestina ni mapambano

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imesisitiza tena kwamba, njia pekee ya kuzikomboa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni maghasibu ni mapambano.

Taarifa ya Hamas iliyotoletwa kwa mnasaba wa Yaumul ardh (Siku ya Ardhi) iliyoadhimishwa kote hapo jana huko Palestina imesema baya kwamba, ardhi za Palestina zitakakombolewa kwa mapambano na muqawama tu.

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imesisitiza tena juu ya kuupinga kikamilifu mpango wa Muamala wa Karne na kueleza kinagaubaga kuwa, hakuna njia itakayopelekea kukombolewa taifa la Palestina ghairi ya mapambano na muqawama.

Tarehe 30 Machi miaka 44 iliyopita, maandamano makubwa yaliyopewa jina la "Yaumul Ardh" au Siku ya Ardhi yalifanyika huko katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu kupinga kuporwa maelfu ya hekari za ardhi za Wapalestina katika mji wa al-Khalil kaskazini mwa Palestina.

Maandamano ya mwaka huu ya Wapalestina ya Siku ya Ardhi hayakufanyika kutokana na kupigwa marufuku ya mikusanyiko ya aina yoyote kufuatia mlipuko wa virusi vya Corona. Kumbukumbu ya mwaka huu ya Siku ya Ardhi imewadia katika hali ambayo, njama za Wazayuni na waitifaki wao za kupora ardhi za Wapalestina zimeshika kasi katika miaka ya hivi karibuni kupitia mipango mbalimbali kama wa Muamala wa Karne ambao umeendelea kulaaniwa kila kona ya dunia.

Tarehe 28 Januari, Rais Trump na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu walizindua mpango huo wa kibaguzi wa Muamala wa Karne katika Ikulu ya White House. 

Kwa mujibu wa mpango huo wa Marekani, Quds Tukufu itakabidhiwa kwa utawala wa Kizayuni; wakimbizi wa Kipalestina hawatakuwa na haki tena ya kurejea katika ardhi za mababu zao na makundi ya muqawama hayataruhusiwa kumiliki silaha.