Brigedia Jenerali Baqeri: Hatua yoyote dhidi ya Iran itajibiwa vikali zaidi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i60133-brigedia_jenerali_baqeri_hatua_yoyote_dhidi_ya_iran_itajibiwa_vikali_zaidi
Kamanda wa Vikosi vya Ulinzi vya Iran amezungumzia harakati za kijeshi za Marekani nchini Iraq na katika eneo la Ghuba ya Uajemi na kueleza kuwa Marekani itakabiliwa na jibu kali iwapo itachua hatua au kutaka kuteteresha usalama wa Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 02, 2020 22:31 UTC
  • Brigedia Jenerali Baqeri: Hatua yoyote dhidi ya Iran itajibiwa vikali zaidi

Kamanda wa Vikosi vya Ulinzi vya Iran amezungumzia harakati za kijeshi za Marekani nchini Iraq na katika eneo la Ghuba ya Uajemi na kueleza kuwa Marekani itakabiliwa na jibu kali iwapo itachua hatua au kutaka kuteteresha usalama wa Iran.

Brigedia Jenerali Mohammad Baqeri ameongeza kuwa Jamhuri ya Kiislamu na majeshi yake yote vinasimamia kwa makini maeneo yote ya mipaka ya nchi kavu, anga na baharini na kufuatilia kikamilifu harakati zote. 

Kamanda wa Vikosi vya Ulinzi vya Iran amesema kuwa harakati za kijeshi za Marekani huko Iraq na katika eneo la Ghuba ya Uajemi zinapigiwa debe na makelele mengi katika vyombo vya habari vya vibaraka wa Marekani dhidi ya wanamuqawama huko  Iraq na kikosi cha wapiganaji wa kujitolea cha wananchi cha al Hashd al Shaabi. 

Brigedia Baqeri Baqeri amesisitiza kuwa viongozi wa Marekani wanafahamu vyema kwamba wananchi wa eneo hili wakiwemo wa Iraq wanapinga kuweko majeshi ya nchi hiyo katika nchi hizo.  

Wanajeshi vamizi wa Marekani nchini Iraq  

Harakati za kijeshi zinazotia shaka za Marekani za kuwahamisha wanajeshi wake huko Iraq sambamba na ripoti zinazosema kuwa Washington inafanya mipango ya kuyashambulia baadhi ya makundi ya muqawama wa Kiislamu na lile la al Hashd al Shaabi, vimeibua wasiwasi ncini Iraq.