HAMAS: Tutaendeleza mapambano dhidi ya utawala haramu wa Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i60975-hamas_tutaendeleza_mapambano_dhidi_ya_utawala_haramu_wa_israel
Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesisitiza kuwa, harakati hiyo itaendeleza muqawama na mapambano yake dhidi ya utawala haramu wa Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 14, 2020 06:32 UTC
  • HAMAS: Tutaendeleza mapambano dhidi ya utawala haramu wa Israel

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesisitiza kuwa, harakati hiyo itaendeleza muqawama na mapambano yake dhidi ya utawala haramu wa Israel.

Ismail Hania amesema kuwa, muqawama unapaswa kuachwa huru ili uweze kukabiliana na mpango wa utawala ghasibu wa Israel wa kuunganisha na ardhi unazozikalia kwa kwa mabavu sehemu ya ardhi za Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesisitiza umuhimu wa umoja na mshikamano na kutobanwabanwa muqawama katika kukabiliana na utawala vamizi wa Israel na maamuzi yanayohusiana na kuunganishwa maeneo ya Palestina na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo ghasibu.

Ismail Hania amesema kuwa, harakati ya Hamas inaunga mkono kwa nguvu zake zote hatua yoyote ile ya kweli na madhubuti inayolenga kukabiliana na utawala haramu wa Israel pamoja na mipango yake ya kupora na kughusubu ardhi za Wapalestina.

Vitongoji vya walowezi wa Kizayuni vilivyojengwa katika maeneo ya Wapalestina

Uporaji wa ardhi za Wapalestina unaofanywa na utawala haramu wa Israel unakwenda sambamba na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na umeshika kasi zaidi tangu Rais Donald Trump aliposhika hatamu za uongozi nchini Marekani.   

Hayo yanajiri katika hali ambayo, hadi sasa hakujachukuliwa hatua yoyote ya kutekeleza azimio nambari 2234 la tarehe 23 Disemba 2016 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka kusitishwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.