Sayyid Nasrullah: Iran imeweza kupiga hatua licha ya vikwazo
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i62072-sayyid_nasrullah_iran_imeweza_kupiga_hatua_licha_ya_vikwazo
Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefanikiwa kupiga hatua za maendeleo na ustawi licha ya vikwazo na mashinikizo ya maadui.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 08, 2020 03:35 UTC
  • Sayyid Nasrullah: Iran imeweza kupiga hatua licha ya vikwazo

Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefanikiwa kupiga hatua za maendeleo na ustawi licha ya vikwazo na mashinikizo ya maadui.

Sayyid Hassan Nasrullah amesema hayo katika hotuba yake aliyoitoa kupitia kanali ya televisheni ya Al-Manar, ambapo ameashiria kuhusu ushindi mtawalia wa kambi ya muqawama na kufeli njama za Marekani nchini Lebanon na katika eneo la Asia Magharibi mwa ujumla.

Amelipongeza taifa la Iran kwa kusimama kidete mkabala wa mashinikizo na vikwazo vya maadui hususan Marekani na kueleza bayana kuwa, "mfumo unaoiongoza Iran umejitosheleza, kwa nini mnaouogopa huu mfumo? Iran iko tayari kuiuzia Lebanon mafuta kwa kutumia sarafu ya pauni ya Lebanon."

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema balozi wa Marekani nchini humo amekuwa akiingilia wazi wazi masuala ya ndani ya nchi hiyo na kwamba nchi hiyo ya Kiarabu inapinga vikali tabia hiyo. Amemhutubu balozi huyo, Dorothy Shea kwa kumwambia: Marekani haina ustahiki wa kuyapa somo mataifa mengine kuhusu haki za binadamu wakati dola hilo la kibeberu ni mkiukaji nambari moja wa haki hizo, mbali na kuunga mkono na kufadhili ugaidi katika eneo. 

Askari wa Hizbullah wa Lebanon

Amesema Marekani ndio utawala dhalimu zaidi duniani na chokochoko zote zilizofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Lebanon zimefanyika kwa uungaji mkono wa Washington.

Sayyid Nasrullah ameihutubu serikali ya Washington kwa kusema, "sera yenu ya kuwabana wananchi wa Lebanon haitakuwa na matokeo mengine ghairi ya kuipa nguvu zaidi Hizbullah na kudhoofisha ushawishi wenu na vibaraka wenu."