Aug 29, 2020 02:37 UTC
  • Muungano wa Fat'h: Trump hana haki ya kuainisha wakati wa kubakia wanajeshi wa Marekani nchini Iraq

Muungano wa al Fat'h katika Bunge la Iraq umetangaza kuwa Rais Donald Trump wa Marekani hana haki ya kuainisha wakati wa kuendelea kuwepo wanajehi wa nchi yake katika ardhi ya Iraq.

Hassan Shakir ambaye ni miongoni mwa viongozi waandamizi wa Muungano wa al Fat'h katika Bunge la Iraq amesema kuwa, Iraq kamwe haijawahi kuiomba Marekani itume wanajeshi wake nchini Iraq. 

Hassan Shakir ameongeza kuwa, Bunge la Iraq lilipasisha uamuzi wa kuwafukuza wanajeshi wa kigeni katika ardhi ya nchi hiyo na uamuzi huo umeungwa mkono na wananchi kwa maandamano yaliyofanyika nchini kote. 

Kiongozi huyo wa Muungano wa al Fat'h amesema kuwa hakuna Waziri Mkuu yeyote wa Iraq aliyewahi kuiomba Marekani itume wanajeshi nchini Iraq na kwamba, Baghdad iliomba msaada wa kilojestiki na kipepelezi. Ameongeza kuwa kutumwa wanajeshi wa Marekani katika ardhi ya Iraq kumefanyika kinyume cha sheria na bila ya kupasishwa na Bunge.

Laana ya Haj Soleimani yaendelea kuwaandama Wamarekani

Tarehe 5 Februari mwaka huu Bunge la Iraq lilipasisha sheria ya kuwafukuza wanajeshi wa Marekani katika ardhi ya nchi hiyo. Uamuzi huo ulichukuliwa baada ya wanajeshi magaidi wa Marekani kumuua shaihidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na aliyekuwa kaimu kamanda wa harakati ya wananchi wa Iraq ya al Hashul Shaabi, Abu Mahdi al Muhandes nje kidogo ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad. 

Kamanda Soleimani alikuwa safarini nchini Iraq kwa mwaliko rasmi wa waziri mkuu wa nchi hiyo.    

Tags