Nov 28, 2020 10:28 UTC
  • Mamluki wa Saudia na Imarati wazidi kutwangana nchini Yemen

Mapigano makali yanaendelea kusini mwa Yemen, baina ya mamluki wa Saudi Arabia chini ya serikali iliyojiuzulu ya Mansour Hadi na mamluki wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati), chini ya Baraza la Mpito la Kusini.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Sputnik, mamluki watano wa Baraza la Mpito la Kusini linaloungwa mkono na Imarati wameuawa katika mapigano ya jana Ijumaa kati yao na wapiganaji wa serikali iliyojiuzulu la Mansour Hadi inayoungwa mkono na Saudi Arabia. Mapigano hayo yanaendelea katika mji wa Zinjibar, makao makuu ya mkoa wa Abyan wa kusini mwa Yemen.

Wapiganaji kadhaa wa Mansour Hadi wakiwemo makamanda wawili wa wapiganaji hao wameshauawa katika mapigano hayo.

Maeneo ya mashariki mwa mji wa Zinjibar huko Yemen yanashuhudia mapigano ya mara kwa mara baina ya mamluki wa Saudia na Imarati. Kiujumla ugomvi baina ya mamluki huo hautarajiwi kumalizika ila kama utamalazika mzozo baina ya Saudi Arabia na Imarati kuhusu nani wa kuwa na ushawishi mkubwa zaidi nchini Yemen, katika maeneo yanayodhibitiwa na mamluki wao.

Mamluki wa Imarati wakipeperusha bendera ya dola hilo vamizi nchini Yemen

 

Mwanzoni mwa mwezi huu wa Novemba pia, televisheni ya Rusia al Yaum ilimnukuu mwandishi wake nchini Yemen akiripoti habari ya kuzuka mapigano makali baina ya mamluki wa Saudia na Imarati katika mkoa wa Abyan wa kusini mashariki mwa Yemen.

Vile vile duru za kieneo ziliiambia televisheni ya al Jazeera ya Qatar kwamba watu wasiopungua wanane waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika saa za awali tu za mapigano hayo. 

Mapigano hayo yalizuka baada ya kujitoa ujumbe wa mazungumzo wa Baraza la Mpito la Kusini mwa Yemen ambalo ni la vibaraka wa Imarati, kwenye mazungumzo ya Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia.

Tags