Israel yaendeleza jinai, yawajeruhi na kuwateka nyara makumi ya Wapalestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i68340-israel_yaendeleza_jinai_yawajeruhi_na_kuwateka_nyara_makumi_ya_wapalestina
Wanajeshi makatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameteka nyara na kujeruhiwa makumi ya Wapalestina baada ya kuvamia nyumba zao na kubomoa vijiji vyao.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 26, 2021 22:04 UTC
  • Israel yaendeleza jinai, yawajeruhi na kuwateka nyara makumi ya Wapalestina

Wanajeshi makatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameteka nyara na kujeruhiwa makumi ya Wapalestina baada ya kuvamia nyumba zao na kubomoa vijiji vyao.

Televisheni ya "al Ikhbariya Souriya" imeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, makumi ya Wapalestina wamejeruhiwa na kutekwa nyara na wanajeshi makatili wa Israel katika maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na wengine kadhaa wamezimia na kubanwa na koo kutokana na gesi za sumu zilizotumiwa na wanajeshi hao madhalimu.

Wanajeshi wa Israel wamevamia kitongoji komoja katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kufyatua mabomu ya kutoa machozi. Wamevamia pia kitongoji kingine cha kaskazini magharibi mwa mji wa Baytul Muqaddas na kutumia risasi za kivita kuwashambulia Wapalestina wa kawaida na kuwajeruhi vibaya.

Bendera ya utawala wa Kizayuni wa Israel

Wanajeshi hao vamizi wa Israel wamevamia pia vitongoji kadhaa katika miji ya Alkhalil, Ramallah, Bayt al Lahm na Nablos huko Palestina na kuteka nyara Wapalestina wakiwa ndani ya nyuumba zao. Kwa uchache Wapalestina 24 wametekwa nyara na wanajeshi makatili wa Israel kwenye maeneo hayo na kupelekwa kusikojulikana.

Wanajeshi vamizi wa Kizayuni wamekivamia pia kijiji cha al Araqeeb huko Beersheba, Palestina, na kuvunja kiholela nyumba za wanakijiji hicho. Tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2021 hadi hivi sasa, wanajeshi wa Israel wameshakivamia mara nne kijiji hicho na kufanya uharibifu mkubwa. 

Kijiji hicho kilijengwa mwaka 1914. Hata hivyo baada ya Wazayuni kuvamia ardhi za Wapalestina mwaka 1948 na kuzipachika jina bandia la Israel, kijiji hicho kimeshavunjwa mara 184, lakini Wapalestina wamesimama imara kukijenga tena na tena kijiji chao.