Mpinzani wa Saudia: Bin Salman ni Saddam mpya Mashariki ya Kati
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i68862-mpinzani_wa_saudia_bin_salman_ni_saddam_mpya_mashariki_ya_kati
Mpinzani mashuhuri wa Saudii Arabia, Umar Abdul Aziz amesema kuwa mrithi wa kiti cha ufalme wa nchi hiyo, Muhammad bin Salman atakuwa Saddam Hussein mpya wa Mashariki ya Kati iwapo ataendelea na kazi na mwenendo wake wa sasa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 09, 2021 22:05 UTC
  • Mpinzani wa Saudia: Bin Salman ni Saddam mpya Mashariki ya Kati

Mpinzani mashuhuri wa Saudii Arabia, Umar Abdul Aziz amesema kuwa mrithi wa kiti cha ufalme wa nchi hiyo, Muhammad bin Salman atakuwa Saddam Hussein mpya wa Mashariki ya Kati iwapo ataendelea na kazi na mwenendo wake wa sasa.

Mpinzani huyo wa utawala wa kifalme wa Saudi Arabia amesisitiza ulazima wa kuuzuliwa Muhammad bin Salman kama mrithi wa kiti cha ufalme wa nchi hiyo.

Umar Abdul Aziz amesema kuwa, eneo la Mashariki ya Kati litashuhudia Saddam Hussein mpya iwapo Bin Salman ataendelea na mwenendo wake wa sasa. Amesema hapingi mageuzi yaliyofanywa na Bin Salman lakini amesisitiza kuwa, marekebisho ndani ya utawala huo wa kifalme yanaweza kufanyika bila ya kutoa roho za wanadamu na kuwafunga jela maelfu ya wengine.

Amesema kuwa Muhammad bin Salman anapaswa kususiwa na kwamba inaoneka kuwa, bado hajapata funzo na somo kutokana na yaliyopita.

Umar Abdul Aziz ametilia mkazo umuhimu wa kuuzuliwa mrithi wa ufalme wa Saudia, Muhammad bin Salman na kusema kuwa, mtoto huyo wa mfalme wa sasa wa Saudi Arabia ni tishio kubwa si kwa Saudi Arabia pekee bali kwa kanda nzima ya Magharibi mwa Asia.

Maelfu ya watoto wa Yemen wameuawa katika vita vya Bin Salman dhidi ya taifa hilo.

Saudi Arabia inaendelea kulaumiwa na mashirika ya kutetea haki za binadamu kutokana na ukandamizaji mkubwa unaofanywa na utawala huo dhidi ya wapinzani, wanaharakati wa haki za binadamu na Waislamu wa madhehebu ya Shia waliowengi maeneo ya Mashariki mwa nchi hiyo. Vilevile inalaumiwa kwa mauaji ya maelfu ya raia wa Yemen katika vita iliyoanzishwa na Bin Salman dhidi ya taifa hilo zaidi ya miaka sita iliyopita.