Wananchi wa Bahrain waandamana kumuunga mkono Sheikh Isa Qassim
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i70454-wananchi_wa_bahrain_waandamana_kumuunga_mkono_sheikh_isa_qassim
Wananchi wa Bahrain jana usiku walijitokeza kwa wingi katika maandamano ya kumuunga mkono Sheikh Isa Qassim katika mkesha wa kumbukumbua ya Mashahidi wa Medani ya Al Fada.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 23, 2021 03:33 UTC
  • Wananchi wa Bahrain waandamana kumuunga mkono Sheikh Isa Qassim

Wananchi wa Bahrain jana usiku walijitokeza kwa wingi katika maandamano ya kumuunga mkono Sheikh Isa Qassim katika mkesha wa kumbukumbua ya Mashahidi wa Medani ya Al Fada.

Waandamanaji waliwaenzi mashahidi wa Al Fada kwa kutangaza uungaji mkono wao kwa Sheikh Isa Qassim, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Bahrain.

Washiriki katika maandamano hayo wamesema hata zama zikirudi nyuma bado wataendelea kumuunga mkono Ayatullah Sheikh Isa Qassim katika Medani ya Al Fada eneo ambalo askari wa utawala wa kiimla wa Bahrain waliwafyatulia risasi wananchi waliokuwa wakiandamana kwa amani.

Ikumbukwe kuwa Mei 2017, maafisa wa usalama wa ukoo wa Aal Khalifa walipojaribu kumkamata Ayatullah Isa Qassim katika Medani ya Al Fada, waandamanaji walikusanyika na kulizuia jeshi kumkamata mwanazuoni huyo. Katika ghasia zilizoibuka waandamanaji kadhaa walipigwa risasi na kuuawa shahidi.

Maandamano dhidi ya mfalme wa Bahrain Hamad bin Isa Al Khalifa

Mwamko wa watu wa Bahrain dhidi ya utawala wa kifalme ulianza Februari 14 mwaka 2011, na ungali unaendelea licha ya utawala huo dhalimu kushadidisha ukandamizaji na utumiaji mabavu dhidi ya wananchi hao wanaotaka mabadiliko.

Tokea Februari 14 mwaka 2011 hadi sasa utawala wa ukoo wa Aal Khalifa umewakamata na kuwafunga jela zaidi ya raia 11,000 kwa visingizio mbali mbali visivyo na maana.